Salah Atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kiume wa Mwaka nchini Uingereza



MSHAMBULIAJI wa klabu ya Liverpool raia wa Misri Mohamed Salah ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu ya Uingereza kutosha kwa Shirikisho la Waaandishi wa Habari za Michezo nchini humo.

Salah mwenye umri wa miaka 29 amekuwa na msimu mzuri akiwa na klabu yake ya Liverpool baada ya kufanikiwa kufumania nyavu mara 22 na kutoa pasi za 13 za mabao kwenye jumla ya michezo 31 ya Ligi Kuu nchini Uingereza huku akiwa na jumla ya mabao 30 na pasi 14 za mabao katika michezo 44 aliyoshiriki kwenye mashindano yote.


Salah amekuwa na msimu mzuri akiwa na jumla ya mabao 22 hadi sasa
Mshambuliaji huyo anatwaa tuzo hiyo ambayo msimu uliopita ilichukuliwa na beki wa kati wa Manchester City Ruben Dias lakini pia Salah ndiye kinara wa mabao wa Ligi Kuu ya Uingereza akiwa na jumla ya mabao 22, mabao matano zaidi ya Son Heung-Min wa Tottenham Hotspurs na Cristiano Ronaldo wa Manchester United.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad