KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Ghana Bernard Morrison sasa ni rasmi kuwa hawezi kwenda nchini Afrika Kusini utokana na kufungiwa kuingia ndani ya nchi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo Barbara Gonzalez amethibitisha hilo rasmi kuwa jitihada zilizofanyika za kumuombea kibali cha kuingia nchini Afrka Kusini zimegonga mwamba.
Barbara alisema:
“Tuliwasiliana na watu wa Mamlaka ya Uhamiaji Afrika Kusini kuomba kupata ruhusa ya kuingia na Morrison, walitueleza sharia zao mtu akivu nja hawezi kupata tena nafasi ya kuingia,”
Morrison akifunga goli dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC
“Wametuambia kutokana na kosa lake Mamlaka haipo tayari kumruhusu kutokana na sharia zilivyo, hivyo ni rasmi sasa Morrison hataenda Afrika kusini. Tutamjulisha kocha ili afahamu hilo na kuona jinsi ya kujipanga kwa mechi ya ugenini bila ya Morrison.”
Klabu ya Simba inatarajiwa kucheza na Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mnamo Aprili 17 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kama.
Mchezo wa marudiano unatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Orlando uliopo jijini Johannesburg Afrika Kusini mnamo Aprili 24 mwaka huu.