Mwongozaji wa series ya Squid Game, Hwang Dong-hyuk, ameweka wazi kuwa msimu wa 2 (season 2) wa series hiyo iliyopata umaarufu mkubwa mwaka jana utakuwa tayari mwishoni mwa 2024 kupitia Netflix.
Akiongea na jarida la Variety, Hwang alisema kuwa kwa sasa anarudi nchini Korea Kusini na mipango ya kuanza kuandika msimu mpya na wapili wa Squid Game, baada ya kuandika filamu yake mpya ya Killing Old People Club, ambayo ameahidi kuwa itakuwa kali zaidi kuliko Squid Game.
Series ya "Squid Game" inakukutanisha na watu wanaofanya maamuzi magumu baada ya maisha yao kutokuwa na ahueni kila uchao, huku mmoja wapo akiwa ni Gi-Hun. Hun ni mhusika mkuu katika series hii, ambaye maisha yake amekuwa akiyaendesha kwa ‘kuunga unga’ tu, huku kazi yake kubwa ikiwa ni kucheza kamali.