Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema magari yaliyotengenezwa chini ya mwaka 2010 yasiingizwe nchini
Amesema “Tanzania haitakiwi kuwa dampo kwa kuleta magari yaliyopitwa na wakati. Bunge letu limeshapitisha Sheria magari yote yanayoingizwa nchini yawe yametengenezwa baada ya mwaka 2010 kuja huku mbele. Huo ni wajibu wa TBS, lazima wajiridhishe na kuelimisha wanaoagiza magari”
Aidha, Waziri Mkuu ameitaka Kampuni ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS) kuimarisha utendaji kazi wake ikiwemo kuacha kuchelewesha ushushaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam
Jamii Forums