Nahodha Msaidizi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amesema watacheza kwa heshima dhidi ya wapinznai wao Orlando Pirates katika mchezo wa Mkondo wa Pili Hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika, utakaounguruma Jumapili (April 24) mjini Johannesburg.
Simba SC inatarajiwa kucheza mchezo huo, baada ya kuanzia nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili (April 17), na kupata ushindi wa bao 1-0 kwa njia ya mkwaju wa Penati kupitia kwa Beki wa Kulia Shomari Kapombe.
‘Tshabalala’ amesema mchezo dhidi ya Orlando Pirates utakua mgumu na wenye ushindani zaidi, tofauti na ilivyokua Dar es salaam, hivyo wachezaji watakaopata nafasi ya kucheza siku hiyo hawana budi kufuata maelekezo ya Benchi la Ufundi chini ya Kocha Franco Pablo Martin.
Mwamuzi Bernard Camill kuamua Orlando Vs Simba SC
“Ukienda ugenini unahakikisha unacheza kwa Plan nyingine ya kupata matokeo, kwa hiyo tunamshukuru Mungu kwa hiki ambacho tumekipata nyumbani, lakini bado tunatakiwa kupambana ili tuweze kufuzu Nusu Fainali.”
“Mchezo wa Afrika Kusini utatupasa tushambulie na kujilinda kwa wakati mmoja, kikubwa tutatakiwa kuwaheshimu sana wapinzani wetu kwa sababu wana timu nzuri” amesema ‘Tshabalala’
Hersi Said: Maandalizi ya 2022/23 yameanza rasmi
Simba SC italazimika kulinda ushindi wake wa 1-0, ama kusaka ushindi zaidi katika mchezo wa Mkondo wa pili ugenini Afrika Kusini siku ya Jumapili (April 24), ili kupata tiketi ya kutinga Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Kwa upande wa Orlando Pirates italazimika kusaka ushindi wa mabao mawili kwa sifuri na kuelendelea, ili kujihakikishia nafasi ya kucheza Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika.