Simba yapewa Waafrika Kusini robo fainali CAF...Mkakati ni Kuwamaliza Kwa Mkapa Mabao Mengi




TIMU ya Simba imepangwa kucheza dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika hatua ya robo fainali kombe la Shirikisho Afrika.

Simba imefuzu hatua ya robo fainali baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye kundi D wakiwa na pointi 10 sawa na vinara wa kundi hilo RS Berkane ya Morocco.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara walifikisha pointi hizo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya US Gendermerie kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi uliopigwa April 3 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kwa upande wa Orlando Pirates wao walimaliza kinara katika kundi B wakiwa na jumla ya pointi 13 nyuma ya Al-Ittihad ya Libya iliyomaliza nafasi ya pili na pointi 11.


Mchezo wa kwanza Simba itaanzia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa April 17, kabla ya kumalizia ugenini nchini Afrika Kusini April 24.

Katika hatua nyingine Al Ahly Tripoli itakutana na ndugu zao wa Libya Al-Ittihad wakati TP Mazembe ya DR Congo itapambana na Pyramids ya Misri.

SAFARI YAO PIRATES

Orlando Pirates ya Afrika Kusini imekuwa na rekodi ya kutoa vipigo kwa timu iwe kubwa au ndogo. Katika mechi sita za hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, vinara hao wa kundi B kwa pointi 13 wameshinda mechi nne, sare moja huku wakipoteza mchezo mmoja mbele ya Al Itihad Tripoli ya Libya ugenini.


Katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini wababe hao wanashika nafasi ya tano wakiwa na pointi 35 katika mechi 23 walizocheza wakishinda nane, sare 11 na kufungwa michezo minne.

Mabingwa hao wa Klabu Bingwa Afrika 1995 na mabingwa mara tisa wa Ligi Kuu kikosi chao kinaongozwa na Kocha Fadlu Davids, huku wachezaji nyota wakiwa ni straika Bandle Shandu mwenye mabao manne kwenye kombe hilo, Kabelo Dlamini mwenye mabao matatu na Terrence Dzvukamanja aliyefunga mawili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad