Mapya yaibuka ! Temmie mwanamuziki wa Nigeria aibuka kumlipua mama yake mzazi ambaye ni mchungaji wa kanisa kwa kukaa kimya wakati akinyanyaswa kingono na baba yake wa kambo, aapa kutohudhuria mazishi ya mama yake akifariki, mama mtu aibuka kumuomba radhi mwanae huyo na kukiri alikosea kutokuchukua hatua mapema
Temmie Ovwasa kwa masikitiko amesema alianza kunyanyaswa kingono na baba yake wa kambo akiwa na miaka 11 hadi akiwa na miaka 17. Akamwambia mama yake mzazi ambaye ni mchungaji wa kanisa lakini badala ya mama yake kuchukua hatua kumnusuru akaanza kumwambia binti yake ni muongo na mwenye matatizo ya akili
Temmie amesema baadaye mama yake mzazi akaona dairy ya huyo mume wake akiwa ameandika hilo tukio la kumnyanyasa kingono Temmie lakini hakuchukua hatua
Amesema yeye kuanza kuitwa mwenye matatizo ya akili alianza kuitwa na mama yake mzazi hivyo hata hashangazwi wala kuwachukulia serious watu mitandaoni wanapomuonaga ana matatizo ya akili kwani Kuna mambo watu huwa wanayahitimisha bila kujua undani wa kitu au anachopitia mtu
Baada ya kueleza hilo mtandaoni, mama yake mzazi alimtumia ujumbe wa kumuomba msamaha binti yake huyo na kusema mwanzo hakumwamini ila sasa anamuamini binti yake. Ambapo binti yake huyo hakumkawiza mama yake akamzodoa kwa kumjibu " Huoni hata aibu" eti leo baada ya kulizungumzia hadharani ndio unaniamini
Temmie pia amemlipua dada yake wa kambo ambaye ni mtoto wa mwanaume husika, dada wa kambo amempigia simu Temmie kumuuliza upo sawa kwanini umeeeza vile. Temi amesema mama yake mzazi na dada yake wa kambo ni wanafiki kwasababu waliujua ukweli na walikuwa na miaka 14 ya kumuomba msamaha lakini wakakaa kimya hadi alipoongea sasa hadharani. Amesema walikaa kimya kwa kuona itawatia aibu lakini hawakufikia yeye itamuathiri kiaai gani huku wakimlinda huyo mwanaume asiyestahili kuitwa mume wala baba
Temmie amesema licha ya mama yake mzazi kuwa mchungaji wa kanisa, lakini pia huyo dada yake wa kambo ni msomi wa masters mwenye elimu ya Sheria na aliwahi kufanya utafiti kuhusu unyanyasaji wa kingono kwahiyo mtu hawezi kuwaelewa