Ommy Dimpoz; ni mkali mwingine wa Bongo Fleva, sema tu anafanya muziki kwa starehe zaidi ambaye amefichua siri ya ni wapi anapopata pesa ambazo amekuwa akizitumia kula bata sehemu mbalimbali duniani na kuendesha magari ya kifahari.
Dimpoz anasema kitu kimoja katika maisha unachotakiwa kujua ni kujiongeza mara baada ya kutengeneza jina ambalo ndilo msingi wa kupata madili.
Dimpoz anasema; “Kujiongeza ni kitu kimoja muhimu sana kwa sababu umeshatengeneza jina; jina lako linakusaidia vipi, unatengeneza vipi michongo na siyo kila kitu ni pesa.
“Mimi ni balozi wa GSM toka 2016, sitaki kukuambia nalipwa shilingi ngapi, lakini nalipwa kila mwezi, lakini pia mimi ni creative director, matangazo yote unayoyaona ya GSM na kuisimamia mitandao yao ya kijamii ni kazi yangu mimi kupitia kampuni yangu, lakini sina haja ya kuja kuwaambia watu…”
GPL