Steve Nyerere Atupa Jiwe Gizani..."Hukumu ni Kazi ya Mungu, Hakikisha Cheo na FEDHA Vinakujengea Mahusiano Mazuri na Watu"

 

Anaandika Steve Nyerere..........''Tumekuwa watu wa kuhukumu na tukisahau kazi hiyo ni ya Mwenyezi Mungu,. Tunajibebesha mamlaka makubwa sana na tunasahau mamlaka madogo ya Maisha yako na family yako yanakushinda,

Yapo mambo tumetendewa na Binadamu wenzetu mpaka unajiuliza huyu ni Binadamu kweli ,Upaswi kuweka tunasemehe maana yote mabaya uliotenda naimani Mungu aliye hai aliyaona na yeye anasema nitakujibia kwa wakati ninao penda mimi.,

Kwenye maisha yetu mambo mengi tunajifunza kutoka kwa Binadamu wenzetu hawa hawa akuna hapa Duniani aliyezaliwa na roho mbaya hakuna ,Hakuna aliyeumbwa na FEDHA hakuna hakuna aliyeambiwa wewe ukizaliwa utakuwa tajiri au utakuwa mh hakuna lakini ukifatilia kwa ndani Mafunzo mengi ya kishetani kibli, tumevitafuta sisi wenyewe na ndomana nasema hakuna jela mbaya kama una hela una cheo lakini huna watu ,..

Leo hii hakikisha cheo na FEDHA vinakujengea watu na mahusiano mazuri na watu,..kumbuka kwenye hii Dunia vyote unavyo vipata utaviacha au ipo siku vitatoka kwako kwenda kwa mwingine ndomana sisi wahenga tuna msemo unasema kutesa kwa zamu.,.,.,..,

Mimi kati ya watu wachache wanaojiamini lakini mara kadhaa pia nahitaji watu waniambie,..Kila kitu kitakaa sawa.,

Maombi yanapokuwa Tabia ,
Mafanikio huwa mtindo wa Maisha.,.

Wote tunajifunza kupitia watu walio tuzunguka, Tabia zao, Roho zao, Majivuno, Dharau ,Kebehi, Utwana, Lakini sisi mazoba au wewe uliyetendewa izo Tabia kumbuka zilikukomaza, zilikufanya ujitambue, Uwe na hofu na Mungu, Lakini kikubwa ulikuwa shule kusoma somo kupitia aidha rafiki yako, ndugu yako, au jirani yako,

Usiogope kujaribu tena
Ila ogopa kuumia tena kwa sababu hiyo hiyo tena." Amenaliza Steve Nyerere

Je kwa ulivyoelewa Ujumbe huo Unamgusa Nani? toa Comment yako Hapa Chini
 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad