Kiungo Mchezeshaji wa Klabu ya Yanga SC Salum Abubakar 'Sure Boy” amesema mechi yao ya jana dhidi ya Azam FC ilikua ngumu kutokana na kila timu ilikua inahitaji alama tatu ili kujiweka mazingira mazuri ya msimamo wa ligi kuu ya NBC.
''Ndugu zangu wa Azam FC walikua wamejiandaa ili kuonesha walichokua nacho na haikuwa rahisi wao kuniachia mimi na mimi kuwaachia wao, ila tunamshukuru mungu tumepata alama tatu tunaukaribia ubingwa'' alisema Sure Boy.