Web

Swali, Je, ni Ubora wa Timu ya SIMBA au Ubora wa Ligi?

Top Post Ad




Maswali yamekuwa mengi kuliko majibu, kwa namna ambavyo Tanzania inapiga hatua kwenye soka la kimataifa ngazi ya klabu, swali linabaki ni ligi bora au muwakilishi bora?

Simply kwangu ni SIMBA ambaye ndie Muwakilishi mzuri kwenye hiyo michuano, ni one army agenda, hilo halina kificho

Tanzania msimu ujao tunapeleka timu nne kwenye michuano ya kimataifa, ambapo tuna jumla ya alama 30.5, ambapo Simba kahusika kwenye alama 28, Namungo alama mbili na Yanga ni 0.5, hii pekee itoshe kukupa picha kuhusu Simba

Kwa points zake peke yake bila timu nyingine tayari Simba anachuana na Libya wenye 28, Nigeria mwenye 26 na Zambia ana 24.5, unajaribu kuvuta picha namna gani Mnyama anavyofanya makubwa kimataifa?

Kwanini Simba na sio timu zingine? Kwanini Simba inafanya vyema zaidi? Wataalam wanasema kitu kuhusu speciality, peculiarity and focus of the project undertaken, Simba wana agenda yao binafsi ambayo matokeo yake ndio faida kwa taifa

Nafasi zimepatikana nne, lakini zinaweza kutetewa?? Watu wengi wanasema timu nyingine ziige kwa Simba, je ni njia rahisi kupita? Na njia ambayo Simba wamepitia kufika hapa walipo?

DIGALA nipo hapa twende taratibu

Kwanza kabisa tunahitaji swali muhimu zaidi, “What are the parameters for football development at Simba? Ndio ni lazima tujue vigezo muhimu viliyoashiria ukuwaji wa mpira ndani ya klabu ya Simba, vipo vigezo takribani nane

Unataka kujifunza kwa Simba? Basi shuka nami taratibu, kuna Utawala, benchi la ufundi, miundombinu, rasilimali, vyombo ya habari, Mashabiki, wadau na wachezaji

Mpaka hapo majibu yangu ni kuwa Simba ni mwakilishi bora na kuwa sio kwamba ligi yetu ni bora, darasa hili litaendelea kuhusu parameters nane ambazo wengine wajifunze kwa Simba

Usiichukie Simba, bali either hate or get motivated💪

WHEN DIGALA SPEAKS YOU LISTEN AND TAKE NOTE

By Shaffih Dauda

Below Post Ad

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.