Tanzania imeshika namba 62 kwenye orodha ya passport zenye nguvu zaidi duniani kwa mwaka 2022 huku Japan na Singapore zikishika namba 1 kutokana na passport zao kuwa na uwezo wa kuingia Nchi nyingi zaidi bila visa ( Nchi 192).
Tanzania imepanda kwa kushika namba 62 mwaka 2022 kutoka namba 77 kwenye orodha ya mwaka 2021 ambapo kwa sasa passport ya Tanzania inaweza kumuingiza Mtu Nchi 36 bila VISA huku Nchi 29 Raia wa Tanzania akitakiwa kupewa VISA baada ya kuwasili na hiyo inafanya jumla ya Nchi ambazo Mtanzania hahitajiki kuomba VISA kwenye balozi zake nchini kuwa 65.
Ripoti hii mpya imesema kwenye kiwango cha kuifikia dunia kwa urahisi (world reach) passport ya Tanzania imefikia kwenye 34% huku Nchi ambazo Mtanzania anahitaji kuomba VISA kabla ya kusafiri zikiwa ni 130.
Unahitaji kufahamu ni Nchi gani ukiwa na Passport unaweza kwenda muda wowote baada tu ya kulipia ticket yako @cielotravelagency ? ikumbatie page hii ya millardayo.