Tazama kutozwa Sh300 milioni mlipuko wa moto



Dar es Salaam. Mamlaka ya Bomba la Mafuta la Tanzania na Zambia (Tazama) itatozwa faini ya Sh300 milioni kutokana na kukiuka sheria za mazingira.

 Hatua hiyo inakuja ikiwa zimepita siku mbili tangu moto ulipounguza ghala la kuhifadhia mafuta ghafi lililopo Kigamboni linalomilikiwa na mamlaka hiyo.

Akizungumza leo Ijumaa Machi 8, 2022 alipotembelea eneo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema amepata taarifa kuwa mamlaka hiyo ilishapewa onyo na maelekezo kuhusu uhifadhi wa mazingira wa eneo hilo lakini haikutekeleza hadi moto ulipotokea.

"Hapa nasikia mlishapewa maelekezo siku nyingi na NEMC kuhusu suala la mazingira, lakini hamkutekeleza, sasa faini ya Sh300 milioni inawasubiri kutoka NEMC," amesema Makalla.


 
Kwa upande wake Meneja Operesheni wa Tazama, Gabriel Mkonde amesema mkandarasi waliyempatia kazi hiyo ana vibali vyote vikiwemo vya NEMC na kuhusu maelekezo ya mamlaka hiyo, amekiri kwamba walipewa tangu mwaka 2020 na kuyatekeleza.

Meneja kutoka NEMC, Hamad Tamiru amewataka Tazama kufika ofisini kwao Jumatatu Machi 11, 2022 na nyaraka zote ili kuzikagua kama kweli wamekidhi vigezo vya maelekezo walioyopewa katika kuifanya kazi hiyo.

Aprili 6, 2022 moto uliunguza ghala la kuhifadhia mafuta ghafi lililopo Kigamboni.

Akitoa maelezo siku ya tukio kwa Waziri wa Nishati, January Makamba aliyetembelea eneo hilo, Meneja Operesheni wa kampuni ya Mohaza inayotunza mafuta ghafi katika eneo hilo, Ramadhani Mambya alisema moto huo umesababishwa na kulipuka kwa mota iliyokuwa ikikoroga mafuta hayo kwa ajili ya kupakuliwa.

Katika hatua nyingine, Makalla ametoa siku saba kwa kamati ya ulinzi ya Wilaya ya Kigamboni kufanya uchunguzi wa mafuta yanayodaiwa kumwagika baharini.

Mafuta hayo yalimwagiga siku moja iliyopita na kuzua mjadala kuhusu uhai wa viumbe vilivyoko baharini.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad