Familia ya Muingereza anayepigana nchini Ukraine ilisema amewaambia kuwa atalazimika kujisalimisha kwa vikosi vya Urusi.
Aiden Aslin, kutoka Newark huko Nottinghamshire, amekuwa akipigana nchini Ukraine tangu alipohamia huko 2018, na kuwa mwanamaji katika jeshi la nchi hiyo.
Kikosi chake hivi karibuni kimekuwa kikiulinda mji uliozingirwa wa Mariupol, ambao umekuwa ukishambuliwa vikali na Urusi.
Mama yake Ang Wood alisema mwanawe alimwambia hana chaguo.
"Alinipigia simu na kusema hawana silaha za kupigana," alisema.
"Ninampenda mwanangu, ni shujaa wangu - walipigana kisawa sawa ."
Bi Wood alisema mtoto wake wa kiume - mfanyikazi wa zamani ambaye alipigana na vikosi vya Wakurdi nchini Syria dhidi ya kile kinachoitwa Islamic State - "alisikika sawa", lakini akatoa wito kwa serikali ya Uingereza kutoa msaada zaidi kwa Ukraine.
"Boris [Johnson] anahitaji kumshusha [Vladimir] Putin," aliongeza.
Brennan Philips, rafiki wa Bw Aslin ambaye pia alizungumza naye kwa njia ya simu, alisema alisikika "mwenye nguvu na mwenye roho nzuri".
"Alinipigia simu na kusema 'hatuna chakula, hatuna vifaa, hatuna risasi , tumezingirwa kabisa, lazima tujisalimishe'," alisema.
"Aiden alikuwa anafahamu vizuri kilichokuwa kikiendelea, akiwa mtulivu sana.
"Hawawezi kutoka nje, hawawezi kupigana kwa hivyo hawakuwa na chaguo.
"Nina uhakika kama wangesalia na risasi wangeipiga."