Ukraine:Mshirika wa Putin Atiwa Mbaroni na Idara ya Usalama ya Ukraine



Ukraine inasema imemkamata mwanasiasa mtoro anayeiunga mkono Urusi Viktor Medvedchuk, anayeonekana kuwa mshirika wa karibu wa Rais Vladimir Putin nchini humo.

Idara ya usalama ya Ukraine SBU ilichapisha picha inayodaiwa kumuonyesha Medvedchuk akiwa amefungwa pingu na amevalia magwanda ya jeshi la Ukraine

Alikuwa chini ya kizuizi cha nyumbani katika mji mkuu wa Kyiv kwa tuhuma za uhaini lakini alitoroka mara baada ya Urusi kuivamia Ukraine Februari 24, 2022.

Medvedchuk, 67, anakanusha kufanya makosa.


Katika hotuba yake ya kila siku kwa taifa siku ya Jumanne kupitia njia ya video, Rais wa Ukrain Volodymyr Zelensky alijitolea kubadilishana, Medvedchuk na wavulana na wasichana wa Ukraine ambao sasa wako katika kifungo cha Urusi.

Idara ya usalama ilisema katika taarifa yake: “Unaweza kuwa mwanasiasa anayeiunga mkono Urusi na kufanyia kazi nchi hiyo kwa miaka mingi.

Medvedchuk, ni mwanabiashara tajiri ambaye anaongoza Jukwaa la Upinzani linalounga mkono Urusi – chama cha Life.


Kwa miaka mingi alivumiliwa katika duru za kisiasa za Ukrainia kwa sababu alionekana kama njia muhimu ya mawasiliano na Kremlin, lakini alishtakiwa kwa uhaini mnamo Mei 2021.

Ameeleza mara kwa mara shutuma dhidi yake kuwa ni “ukandamizaji wa kisiasa”.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad