Uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili umepewa miezi miwili kujitafakari kuhusu uwezo wao wa kusimamia ubora wa Huduma za Afya, hiyo ni kutokana na malalamiko yanayotolewa na Wananchi wanaopewa huduma katika hospitali hiyo
Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema hayo baada ya Kikao cha ndani kilichomshirikisha Mganga Mkuu wa Serikali, Viongozi wa Hospitali za Taifa za Kanda, Mikoa na Waganga Wakuu wa Dar es Salaam, leo Aprili 4, 2022
Pia, Waziri Mollel ameutaka Uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha unakuja na suluhu za kudumu za upatikanaji wa huduma bora kwa Wananchi