Upinzani Uingereza wahoji kukamatwa wanajeshi wao Ukraine



Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Uingereza, Emily Thornberry, ameishtumu nchi yake kwa kuruhusu askari wake kushiriki mstari wa mbele katika mapambano yanayoendele Ukraine dhini ya vikosi vya jeshi la Urusi.

Thornberry amesema katika mahojiano na Sky News akihoji mstakabari wa wanajeshi wa Uingereza Shaun Pinner na Aiden Aslin waliokamatwa na vikosi vya Urusi huko Ukraine.

"Haifai kwa Waingereza kuhusika katika vita vya Ukraine na hawapaswi kwenda huko,” Thornberry alisema. "Tunaunga mkono watu wa Ukraine. Tumekuwa tukitoa msaada linapokuja suala la mafunzo. Tumetoa usaidizi katika masuala ya silaha, na tunatoa usaidizi kwa kuwawekea Urusi vikwazo.

"Na tunapaswa kutoa msaada zaidi kwa wakimbizi kuingia Uingereza. Hizi ndizo njia ambazo tunaamini zinaisaidia Ukraine na tunafanya hivyo kwa mshikamano na washirika wetu wengine.


 
Kuhusu hali ya sasa na Waingereza waliotekwa, Thornberry alisema "Tunapaswa kufanya mazungumzo na Urusi ili kujaribu kuwarudisha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad