Urusi inapanga Awamu ya Pili ya Kipigo Ukraine



Urusi inatarajia kuanzisha awamu ya pili ya kampeni ya kivita dhidi ya Ukraine siku chache zinazokuja, ambapo wanajeshi wa Ukraine wakizunguka maeneo tofauti ya wilaya zilizoathirika zaidi ili kukagua usalama.

Wanajeshi wa Urusi walifyatua makombora katika miji iliyoathirika zaidi ambayo ni Kyv, Kaskazini mwa Ukraine, wakielekea Belarus.

Kwa mujibu wa maafisa wawili wa Marekani ambao ni katika kundi la maafisa wanaowakagua warusi, kwa sasa Urusi inajipanga kuanzisha makombora na milipuko wakilenga zaidi Mji wa Donbas na Kusini mwa Ukraine.

Shirika la habari la NBC linasema kuwa hata kama wanajeshi wa Urusi wanajipanga kuanzisha vita kwa awamu ya pili, bado ukweli ni kuwa Ukraine na Urusi zimeendelea kupigana kwa muda mrefu maeneo ya Mashariki na Kusini.


 
Wiki iliyopita Uongozi wa Rais Biden wa Marekani ulitangaza kutuma silaha mara elfu arobaini kwa Ukraine lakini kwa matumizi makubwa ya Ukraine ya Silaha, hizo zinaweza kudumu kwa muda wa siku 7 na maafisa wa kimarekani wanaendelea kuwasiliana na Marekani kutuma silaha zaidi ili Majeshi ya Ukraine isiishiwe pale ambapo awamu ya pili itaibuka.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad