Urusi "Malipo ya gesi lazima yapitie benki za Urusi"



Rais Vladmir Putin alihutubia taifa akisema nchi za Magharibi zitajaribu kutafuta sababu nyingine za kuiwekea vikwazo nchi yake na kwa hivyo ameitaka nchi yake kulenga katika kuzinusuru nafasi za ajira na kutengeza mpya

Russland | Gazprombank
Rais Putin ametishia kusitisha mikataba ya kusambaza barani Ulaya theluthi moja ya gesi yake kama hawatalipwa katika sarafu ya kirusi. Hiyo ndiyo hatua yake ya kwanza muhimu mpaka sasa inayoonesha kulipa kisasi vikwazo vikali alivyowekewa na nchi za Magharibi kuhusiana na uvamizi wake nchini Ukraine

Serikali za Ulaya zimepinga sharti hilo alilosema muda wake wa mwisho ni leo Ijumaa, huku mpokeaji mkubwa wa gesi ya Urusi barani Ulaya, Urusi, ikiita "usaliti”. Moscow hata hivyo, ilitoa utaratibu kwa wanunuzi kutumia sarafu ya kirusi ya roubles kupitia benki ya Urusi.

Ukraine | Angriff auf Kukhari | Zerstörung
Mashambulizi yanaendelea viungani mwa Kyiv


Mzozo wa nishati una madhara makubwa barani Ulaya wakati maafisa wa Marekani wakiendeleza kuuzunguka ulimwengu ili kuendeleza shinikizo kwa Putin kusitisha uvamizi wake wa wiki tano na ambao umesababisha Zaidi ya watu milioni 4 kuikimbia Ukraine.

Ulaya inataka kuondokana na nishati ya Urusi lakini hiyo inaharatisha Zaidi kuongezeka kwa bei za Mafuta. Huku akikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa jeshi la Ukraine, Putin amecheza mojawapo ya karata zake kubwa katika masharti yake kwa wanunuzi wa nishati barani Ulaya "Ili kununua gesi asilia ya Urusi, lazima wafungue akaunti za sarafu ya rouble katika mabenki ya Urusi. Ni akaunti hizi zitakazotumika kulipia gesi inayosambazwa kuanzia Aprili mosi mwaka huu. Kama malipo hayo hayatafanywa, tutazingatia hili kuwa ukiukaji kwa upande wa wanunuzi."

Mapambano yaliyo mbele
Kwenye mazungumzo wiki hii, Moscow ilisema itapunguza mashambulizi yake karibu na mji mkuu Kyiv na katika upande wa kaskazini kama ishara ya nia njema na kulenga katika kulikomboa eneo la kusini mashariki la Donbas. Kyiv na washirika wake wanasema badala yake Urusi inajaribu kujipanga upya baada ya kupata hasara kutoka kwa mashambulizi ya Ukraine ambayo yamesababisha kukombolewa kwa viunga vya mji mkuu pamoja na maeneo ya kimkakati ya kaskazini mashariki na kusini magharibi.


Katika hotuba yake ya usiku wa manane, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alionya kuhusu mapambano yaliyoko mbele katika eneo la Donbas na mji wa bandari wa kusini uliozingirwa wa Mariupol.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad