Urusi Yakamilisha Kuyaondoa Majeshi Yake Kutoka Kyiv na Chernihiv, Marekani Wafunguka



Maafisa wa idara ya ulinzi ya Marekani wamesema kuwa hatua ya Urusi kujiondoa katika mikoa ya Kyiv na Chernihiv sasa imekamilika.

“Vikosi vya Urusi karibu na Kyiv na Chernihiv vimekamilisha kujiondoa katika eneo hilo ili kuungana tena na kurejea Belarus na Urusi,” afisa wa Pentagon aliwaambia waandishi wa habari Jumatano.

“Hatuonyeshi vikosi vya Urusi ndani au karibu na Kyiv au ndani au karibu na Chernihiv,” msemaji wa Pentagon John Kirby baadaye aliongeza, akisema kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin “amefikia sifuri ya malengo yake ya kimkakati”.

“Kwa kweli anadhibiti tu vituo vidogo vya watu …. Hawajachukua Kharkiv.”


 
Inakuja siku chache baada ya Urusi kutangaza kwamba itaelekeza nguvu zake katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine.

Afisa mkuu wa Pentagon, akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, alisema kwamba wanajeshi wa Urusi wanaweza kurudi Kyiv katika siku zijazo, na kwamba bado haijafahamika ikiwa wanajeshi wanaorejea ndio watakaotumwa tena

Kulingana na Taasisi ya Utafiti wa Vita ,vitengo vya Urusi vinavyorudi kutoka karibu na Kyiv vina uwezekano wa “kupata tena ufanisi wa vita kwa muda”.


Kati ya vikosi 130 vya Urusi ambavyo vimetumwa Ukraine, zaidi ya 80 bado vimesalia nchini, afisa huyo alisema.

Shirika la habari la Associated Press, likimnukuu afisa wa ulinzi wa Marekani, akisema kwamba idadi ya wanajeshi wa Urusi walioondoka ni takriban watu 24,000
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad