Urusi yatangaza kujisalimisha kwa wanajeshi zaidi ya elfu moja huko Mariupol



Picha ya satelaiti ya jiji la Mariupol, lililozingirwa na kushambuliwa kwa mabomu tangu mwanzo wa vita, Aprili 9, 2022.
Picha ya satelaiti ya jiji la Mariupol, lililozingirwa na kushambuliwa kwa mabomu tangu mwanzo wa vita, Aprili 9, 2022. via REUTERS - MAXAR TECHNOLOGIES
Katika siku ya 49 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Rais wa Marekani Joe Biden ametaja vitendo vya Urusi nchini Ukraine kuwa ni "mauaji ya halaiki", na kuongeza kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin "(alikuwa) akijaribu kutokomeza Ukraine".

Akizungumza katika hafla moja huko Iowa, alipokuwa akielezea kupanda kwa gharama ya nishati kutokana na mzozo huo, Biden aMebeini kwamba Putin anatekeleza mauaji ya halaiki dhidi ya Ukraine. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, ambaye amekuwa akiwahimiza viongozi wa magharibi kutumia neno hilo kuelezea uvamizi wa Urusi katika nchi yake, amepongeza kauli hiyo ya rais wa Marekani.

Kwa upande mwingine zaidi ya wanajeshi elfu moja wa Ukraine wamejisalimisha kwa vikosi vya Urusi katika mji wa Mariupol, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema leo Jumatano. Siku ya Jumanne, mamlaka za kikanda kusini mashariki mwa Ukraine zilitathmini idadi ya vifo vya takriban watu 20,000 katika bandari ya kimkakati ya Bahari ya Azov iliyozingirwa kwa wiki kadhaa ambapo mapigano sasa yamejikita katika eneo kubwa la viwanda.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anatarajiwa mjini Kyiv kwa "maamuzi ya kivitendo" ikiwa ni pamoja na utoaji wa silaha nzito kusaidia Ukraine katika kukabiliana na mashambulizi ya Urusi, mshauri wa rais wa Ukraine amesema leo Jumatano. Wakuu wa nchi za Poland na Baltic pia wanaenda katika mji mkuu wa Ukraine "kumuunga mkono" rais wa Ukraine "wakati wa maamuzi kwa nchi hii".


 
Ukraine haitafungua eneo hata moja la usalama wa kiutu  leo Jumatano, Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk amesema, kutokana na "kiwango cha hatari". Anaishutumu Urusi kwa "kukiuka kanuni za sheria za kimataifa".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad