Urusi Yatoa Onyo Kali kwa Marekani Kuacha Kuipatia Misaada ya Kivita Ukraine




Sehemu ya msaada wa silaha za kivita kutoka Marekani na (NATO) ukiwasili nchini Ukraine
URUSI  imeionya Marekani na mataifa mengine washirika wengine kuacha mara moja kusambaza silaha kwa Ukraine.

Onyo hilo lilikuja katika barua rasmi ya kidiplomasia kutoka Moscow, ambayo nakala yake imepitiwa na vyombo vya habari nchini Marekani.

Barua hiyo ya kidiplomasia ya kurasa mbili iliyotumwa kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na ubalozi wa Urusi mjini Washington inaonya kwamba shehena za silaha za Marekani na Nato “zinaongeza mafuta” katika mzozo wa Ukraine, na inaweza kusababisha kile wanadiplomasia wa Urusi wanataja kuwa matokeo ‘yasiotabirika’.

Barua hiyo Ilitumwa siku ya Jumanne, mara tu baada ya habari baada ya Marekani kutangaza kupeleka shehena ya silaha Ukraine.


 
Afisa mkuu wa utawala wa Marekani alinukuliwa akisema onyo hilo linaweza kuonekana kama makubaliano na Urusi kwamba msaada wa kijeshi wa Marekani na Nato kwa Ukraine ulikuwa na ufanisi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad