VITA YA URUSI NA UKRAINE: Marekani imesema inaamini Mali nyingi za Rais wa Urusi, Vladimir Putin zimefichwa na Wanafamilia. Kauli hiyo inakuja kufuatia vikwazo vipya vilivyotangazwa dhidi ya Watu wa karibu wa Putin wakiwemo Mabinti zake wawili
Taarifa ya Marekani imemtaja Katerina Vladimirovna Tikhonova kama Mkurugenzi kwenye Masuala ya Teknolojia ambaye kazi yake inasaidia Serikali ya Urusi na Sekta ya Ulinzi
Binti mwingine wa Putin, Maria Vladimirovna Vorontsova anatajwa kuongoza Programu zinazofadhiliwa na Serikali ambazo zimepokea Mabilioni ya Dola
#JamiiForums