La primera ministra de Finlandia, Sanna Marin (derecha), y la lÃder sueca Magdalena Andersson en Estocolmo.
Mwishoni mwa mwezi Januari, wanajeshi wa Urusi walipokusanyika kwenye mpaka wa Ukraine na wengi bado wana shaka iwapo Urusi ingethubutu kuivamia, Waziri Mkuu wa Finland Sanna Marin alisema "hakuna uwezekano mkubwa" kwamba nchi yake itaomba kujiunga na NATO.
Alieleza kuwa hatua hiyo itakuwa na athari kubwa sana na kwamba vikwazo vitakuwa "vikali sana."
Lakini baada ya uamuzi wa Rais wa Urusi Vladimir Putin kuivamia Ukraine, kwa kisingizio cha "kuituliza" nchi hiyo, maono yake yamechukua mkondo mkubwa.
Siku ya Jumatano, Finland ilizindua mjadala ambao unaweza kuona taifa la Uskandinavi kuomba kujiunga na muungano katika muda wa wiki.
Nchi jirani ya Uswidi ilichukua mkondo sawa na huo, wakati chama tawala cha Social Democratic, ambacho kwa muda mrefu kimepinga kujiunga na NATO, kilipofichua kwamba kinatafakari upya msimamo wake kufuatia shambulio la Urusi.
"Wakati Urusi ilipoivamia Ukraine, msimamo wa usalama wa Uswidi ulibadilika," chama kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa Uswidi Magdalena Andersson kilisema katika taarifa Jumatatu.
Moscow imeweka wazi kuwa inapinga upanuzi wowote wa muungano huo.
Msemaji wa Putin, Dmitri Peskov, alionya kuwa umoja huo "sio aina hiyo ya muungano unaohakikisha amani na utulivu, na upanuzi wake zaidi hautaleta usalama wa ziada katika bara la Ulaya."
Wiki iliyopita, Peskov alitishia kwamba Urusi italazimika "kusawazisha hali" na hatua zake ikiwa Uswidi na Finland zitajiunga na NATO.
Gráfico
Na mwezi Februari, Maria Zakharova, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, alionya kuhusu "matokeo ya kisiasa na kijeshi" ikiwa nchi zitajiunga na umoja huo.
"Katika wiki zijazo"
Licha ya maonyo mengi ya Urusi, Robert Dalsjö, mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijeshi katika Taasisi ya Utafiti ya Ulinzi ya Uswidi, anasema kwamba Finland imedhamiria kujiunga na NATO na imeanza mchakato wa haraka na uliopangwa kufanya hivyo.
"Hakuna mazungumzo tena marefu ya miezi, lakini ya wiki, na Uswidi inajaribu kufuata Finland katika mchakato huo," mtaalam aliiambia BBC Mundo.
Gazeti la Uswidi la Svenska Dagbladet liliripoti Jumatano kwamba waziri mkuu wa Uswidi amedhamiria kuomba kujiunga na NATO na kwamba serikali yake inapanga kuwasilisha ombi hilo katika mkutano wa kilele wa Madrid ambao muungano wa kijeshi unatarajia kufanya mwishoni mwa Juni.
Ripoti hii ilifichuliwa siku hiyo hiyo ambapo viongozi wa Finland na Uswidi walikutana huko Stockholm, mji mkuu wa Uswidi, kujadili maswala ya usalama wa kikanda baada ya uvamizi wa Urusi huko Ukraine.
Maelezo ya picha, Sanna Marin, Waziri Mkuu wa Finland.
Baada ya mkutano huo, Sanna Marin alithibitisha kuwa nchi yake itaamua kama itaomba kujiunga na NATO "ndani ya wiki chache."
"Sitatoa aina yoyote ya ratiba ya ni lini tutafanya maamuzi yetu, lakini nadhani itafanyika haraka sana," alisema.
Wiki kadhaa mapema, Marin alihalalisha badiliko lake la moyo kuhusu NATO kwa kusema kwamba "Urusi sio jirani tuliyofikiria kuwa yuko hivyo."
Mwisho wa kutoegemea upande wowote
Kijadi, nchini Finland na Uswidi kila mara kulikuwa na upinzani mkubwa wa jumla wa kujiunga na NATO.
Wasweden walitaka tu kuendelea kutumia msimamo wao wa kutoegemea upande wowote, wakati tangu kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia, Finland ililazimika kushawishi Umoja wa Usovieti kwamba haikuwa tishio kwa nguvu hiyo na ikachukua msimamo.
Hapo zamani, Urusi ilikuwa tayari imeivamia Finland mara kadhaa na hata kuichukua kama eneo dogo linalojitegemea tangu mwanzo wa karne ya 19 hadi mwaka 1917. Uvamizi wa mwisho ulikuwa Novemba 1939, miezi michache baada ya kuanza kwa Vita vya Kidunia vya pili katika vita ambayo iliitwa Vita Baridi, lakini upinzani wa kijeshi dhidi ya uvamizi huo, uliruhusu nchi kubaki huru kutoka kwa utawala wa Soviet na Ukomunisti.
Finland ilisalia kutoegemea upande wowote na sera za kigeni zikafanya isijiunge na NATO wala Mkataba wa Warsaw, licha ya ukweli kwamba Moscow ilitaka ijiunge na muungano wake.
El secretario general de la OTAN, Jens Stoltenberg (centro), el ministro de Asuntos Exteriores de Finlandia, Pekka Haavisto, y la ministra de Asuntos Exteriores de Suecia, Ann Linde, celebran una conferencia de prensa en la sede de la OTAN, en Bruselas, el 24 de enero de 2022.
Hata hivyo, matukio ya Ukraine yamesababisha mabadiliko makubwa katika nchi hizi za Nordic.
Kwa mtazamo wa Ukraine
Katika mataifa yote mawili, uungwaji mkono wa umma kwa Uanachama wa NATO umeongezeka kwa kasi katika miezi ya hivi karibuni.
Ijapokuwa hapo awali wengi walitilia shaka au walipinga tu, sasa karibu 60% ya Wafinland na karibu 50% ya Wasweden sasa wanaunga mkono, kulingana na kura za maoni.
"Ukraine imekuwa ikipokea msaada wa kijeshi, kiuchumi na kimaadili, lakini hakuna nchi (ya NATO) itaingia vitani kwa ajili ya nyingine ambayo si mwanachama," anaeleza mtaalamu wa Uswidi.
"Itakuwa nzuri" Ivo Daalder, mtaalamu wa usalama wa Ulaya na mwenyekiti wa Baraza la Masuala ya Ulimwenguni huko Chicago, ana uhakika kwamba nchi zote za NATO zitakaribisha maombi ya uanachama wa Finland na Uswidi.
"Itakuwa nzuri sana kama wangejiunga.
Ni washirika wa karibu wa NATO na wamekuwa kwa miaka mingi," mtaalamu huyo wa Marekani anaiambia BBC Mundo.
Ivo Daalder (centro) junto al secretario de Defensa de EE.UU., Chuck Hagel (izquierda), y el ministro de Defensa de Georgia, Irakli Alasania en junio de 2013.
Maelezo ya picha, Ivo Daalder (katikati) akiwa na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel (kushoto) na Waziri wa Ulinzi wa Georgia Irakli Alasania mnamo Juni 2013
"Kwa kuongeza, wamekaa pamoja na wanachama wengine wa NATO katika makao yao makuu huko Brussels kwenye mikutano yote mikuu ya muungano."
Daalder, ambaye alikuwa balozi wa zamani wa Marekani katika NATO kuanzia mwaka 2009 hadi 2013, anaongeza kuwa Wafinland wanajua kwamba mazingira yamebadilika na kwamba kugawana mpaka wa kilomita 1,340 na Urusi kunawafanya kuwa hatarini zaidi.
Maafisa wa ulinzi wa Marekani wamesema uvamizi wa Moscow dhidi ya Ukraine ulikuwa "kosa kubwa la kimkakati" ambalo huenda likachochea upanuzi wa NATO.
Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, mazungumzo kati ya viongozi wa NATO na mawaziri wa mambo ya nje wa Finland na Sweden tayari yalikuwa yamefanyika wiki iliyopita.
Wataalam wanatarajia kwamba majirani wa Nordic yaani Skandinavia watawasilisha ombi hivi karibuni na kwamba Washington itaunga mkono, ambayo itachukua idadi ya wanachama wa muungano wa kijeshi hadi 32.
Matumizi zaidi ya ulinzi
NATO iliundwa mwaka 1949 ili kukabiliana na tishio la upanuzi wa Soviet, ingawa idadi ya nchi za Ulaya ya Mashariki zilizokuwa za kikomunisti zimejiunga tangu kuanguka kwa Ukuta wa Berlin.
Maelezo ya picha, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alimhakikishia Magdalena Andersson kwamba Ulaya ingeitetea Sweden ikiwa Urusi itaishambulia nchi hiyo.
Wanachama wanakubali kuja kusaidiana iwapo kuna shambulio la silaha dhidi ya mwanachama mwingine yeyote.
Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine sio tu umeongeza uungwaji mkono kwa NATO nchini Finland na Uswidi, pia umesababisha Helsinki na Stockholm kuongeza matumizi yao ya ulinzi.
Siku ya Jumatatu, mamlaka ya ilitangaza mpango mpya wa kutenga euro milioni 14 (dola milioni 15) kununua ndege zisizo na rubani kwa jeshi.
Na mwezi uliopita, maafisa wa Uswidi walisema wataongeza matumizi ya ulinzi kwa kroner bilioni 3 (dola milioni 317) mnamo 2022.
Finland inashirikishana mpaka wa kilomita 1,340 na Urusi na kufuatia uvumi kwamba Helsinki na Uswidi zinapanga kujiunga na NATO, ripoti zimeibuka kuwa Moscow ilianza kuhamisha vifaa vya kijeshi kuelekea mpaka wake na Finland.
Lakini maafisa wa Marekani walikanusha kuwa hawakuona chochote kuthibitisha ripoti hizi.
"Urusi haina tena uhuru"
Balozi wa zamani wa NATO Ivo Daalder hana shaka kwamba muungano wa Atlantiki ungefaidika kutokana na upanuzi.
"Wafinland na Wasweden wana uwezo mkubwa wa kijeshi. NATO itapata washirika wawili ambao wangesaidia kulinda eneo kutoka kwa wanachama wengine wa NATO," anafafanua.
Chanzo cha picha, Getty Images
El secretario general de la OTAN, Jens Stoltenberg.
Maelezo ya picha, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg.
Wakati wengi wakihofia kwamba Urusi itashambulia majirani zake wa Skandinavia mara tu watakapofanya nia yao ya kujiunga na muungano wa kijeshi, Daalder anasema wote tayari wanalindwa na kuwa wanachama wa Umoja wa Ulaya.
Mwishoni mwa mwezi Machi, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz alibainisha kuwa Uswidi inaweza kutegemea "nchi nyingine za Ulaya kuja kujitetea katika tukio la mashambulizi ya Kirusi, ingawa nchi hiyo si mwanachama wa NATO.
Kufuatia mkutano huko Berlin na Waziri Mkuu wa Uswidi Magdalena Andersson, Scholz alisema EU imeunda kifungu cha usaidizi wa pande zote katika mkataba wake na kwamba kifungu hicho "kitachukuliwa kwa uzito mkubwa" ikiwa kutatokea shambulio dhidi ya Uswidi.
Kushindwa kwa Urusi
Kwa Robert Dalsjö, vitisho vya Kremlin vinaonyesha tu "kuchanganyikiwa na kutoridhika" kwa Urusi.
"Urusi haiku tena huru kwa sababu vikosi vyake viko katika vita vikali nchini Ukraine, kwa hivyo haitaweza kulipiza kisasi dhidi ya Finland au Sweden," anafafanua.
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg aliahidi wiki iliyopita kwamba muungano huo ungetafutia ufumbuzi Finland na Sweden katika "kipindi cha mpito".
Tutatafuta njia za kushughulikia maswala yoyote ambayo unaweza kuwa nayo kuhusu kipindi kati ya uwezekano wa kutuma maombi na uidhinishaji wa mwisho."
Nchi zote mbili zimepokea hakikisho kutoka kwa Katibu Mkuu wa NATO, pamoja na jumbe za kuungwa mkono na wanachama mbalimbali, zikiwemo Marekani, Uingereza, Ujerumani na Ufaransa.
Na wakati Helsinki na Stockholm zitaamua kujiunga na muungano wa kijeshi wa Magharibi, wataalam wanakubali kwamba vita vya Ukraine tayari vimesababisha kushindwa kwa Kremlin.
Badala ya kugawanya NATO na kumaliza uwezekano wa upanuzi wake, inaonekana kuwa imeipa nguvu kubwa.