Dar es Salaam. Wakili wa kujitegemea, Peter Madeleka amedaiwa kukamatwa na watu wanaodaiwa kuwa Polisi na kumpeleka katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani jijini hapa.
Hata hivyo, msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime alipoulizwa kwa simu, alisema hana taarifa za kukamatwa wakili huyo.
Juhudi za kuwatafuta makamanda wa Kanda Maalum na Mkoa wa Ilala hazikufanikiwa baada ya simu zao kuita bila kupokelewa.
Hata hivyo, Wakili wa Madeleka, Paul Kisabo alituma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter akisema: "Polisi wametoka kufanya upekuzi Hotel aliyofikia @PMadeleka Dar es Salaam muda huu."
Lakini Wakili Kisabo amesema alizuiwa kuingia ndani kushuhudia upekuzi huo.
Baada ya hapo Polisi hapo waliondoka na Wakili Madeleka.
Awali, Paul Kisabo amesema alizuiwa kumwona mteja wake alipofika ofisi ya Wizara ya Mambo ya Ndano.
Kwa mujibu wa Wakili Kisabo, Madeleka alikamatwa na watu hao alipokuwa kwenye eneo la kuegesha magari la Hoteli ya Serena.
Mkurugenzi wa masoko wa hotel hiyo, Seraphine Lisala alipoulizwa kuhusu suala hilo alikiri kuwepo kwa Madeleka hotelini hapo.
“Huyu mtu ni kweli alikuwepo hapa hotelini leo (jana), lakini aliondoka na hakuna hizo taarifa za kutekwa. Kama kuna tatizo hilo litakuwa limetokea nje ya Serena,” kilieleza chanzo hicho.
Hivi karibuni Wakili Madeleka aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter akidai kuwepo kwa watu wanaotishia kumuu