Watatu mbaroni wakituhumiwa kutorosha madini




Bariadi. Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limewakamata watu watatu kwa tuhuma za kutorosha gramu 14.4 za madini ya dhahabu.

Taarifa ya kukamatwa kwa watu hao imetolewa leo Jumanne Aprili 19, 2022 na ofisa madini wa mkoa huo, Aman Msuya.

Msuya amesema kuwa watu hao wamekamatwa baada msako uliofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama kutokana na tetesi kuwa kuna dhahabu inatoroshwa kwenda Kenya bila utaratibu.

"Wafanyabiashara wanachokifanya wananunua dhahabu kwa magendo na hatuoni taarifa zake licha ya kuwa wamepewa fomu za kujaza taarifa tangu kwenye mwaro hadi kwenda soko kuu wanapokuwa hawazijazi maana yake dhahabu haijafika sokoni," amesema Msuya.


 
Kwa mujibu wa kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Shedrack Masija amesema watuhumiwa hao wapo mahabusu kwa ajili ya taratibu za kisheria na tayari wamewasiliana na ofisi ya madini katika muendelezo wa oparesheni hiyo.

Akizungumza baada kuwatembelea watuhumiwa hao mahabusu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila amewashauri kuwa wawazi na kutoa ushirikiano kwa polisi ili kubaini mtandao wa wanaofanya biashara hiyo.

"Bado nyinyi ni washukiwa usalama wenu ni kutoa taarifa sahihi msipotoa taarifa sahihi mtabaki mahabusu mpaka tutakapo jiridhisha kwamba hamhusiki na kibaya ninajua nyie mmetangulizwa ila kwa nyuma yake kuna watu wanaofanya hii biashara" amesema Kafulila.


Amemuagiza kamanda wa polisi mkoa huo kuhakikisha wanafanya oparesheni maalumu katika maeneo yote ya migodi katika mkoa huo ili kuzuia utoroshaji huo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad