Watu Kadhaa Wateketea kwa Moto Kutokana na Mripuko wa Kiwanda cha Mafuta Nigeria

Watu kadhaa wanahofiwa kuteketea kwa moto kufuatia mripuko uliotokea usiku katika kiwanda kinachochakata mafuta kinyume cha sheria Kusini mwa Nigeria.Polisi imethibitisha kutokea kwa mripuko huo lakini haikutoa maelezo zaidi ya watu walioathirika. 

Fyneface Dumnamene, mkurugenzi mtendaji wa kituo cha vijana na utetezi wa mazingira, amesema, miili kadhaa ilioungua kiasi cha kutotambulika ilizagaa chini, huku wengine waliojaribu kujiokoa maiti zao zikionekana kuning'inia kwenye matawi ya miti. 

Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kuwa zaidi ya watu 100 wameuawa katika mripuko huo wa hivi karibuni nchini Nigeria, ambayo ni mzalishaji mkubwa wa mafuta ghafi barani Afrika. 

Miripuko ya mabomba ya mafuta nchini humo ni jambo la kawaida kutokana na uduni wa miundombinu pamoja na kuhujumiwa kwa mabomba ya mafuta ili kuiba petroli na kuiuza kwa magendo. Mamia wameuawa siku za nyuma kutokana na kuiba na usafishaji haramu wa bidhaa za petroli.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad