Waziri wa Nishati, January Makamba amefanya Mkutano wa pamoja na Waagizaji na Wasambazaji wa Mafuta Nchini leo Jumatano tarehe 06 April, 2022.
Katika Mkutano huo pamoja na mambo mengine waliojadili amesema kuna shehena ya kutosha kwenye maghala yaliyopo ndani, na yale ambayo yanashushwa Bandarini.
"Tunayo mafuta ya kutosha kutumika kwa takriban siku 27. Pia, Serikali imeshaagiza mafuta yatakayotumika Mwezi wa Tano na wa Sita ambayo yapo kwenye Mchakato.”
#TimesFMDigital