Yanga Waipa Heshima Wanayostahili Simba

 


Baadhi ya wapenzi wa Yanga wamejitokeza hadharani kuipongeza Klabu ya soka ya Simba kufuatia hapo jana kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.


Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram wa aliyewahi kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga SC, Dismas Ten amesema kwa kile walichokifanya jana kwa kuinyuka US Gendarmerie kwa kuipa kipigo cha bao 4-0 na kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.


''Kilichofanyika jana kwa Mkapa ndio maana na tafsiri halisi ya kuitwa timu kubwa, amini nawaambia ukiiondoa TP Mazembe, timu nyingine iliyofanikiwa sana kimataifa kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati ni Simba. Kila la Kheri mtani huko uendako, na sisi tutakuja Inshaallah.'' Ameandika Dismas Ten aliyewahi kuwa Afisa Habari wa Yanga.


Mabao ya Simba katika mchezo huo yamefungwa na Sadio Kounate, Chris Mugalu aliyefunga mara mbili na bao moja US Gendermerie walijifunga. Ushindi huu umewafanya Wekundu wa msimbazi kufikisha alama 10 na wamemaliza nafasi ya pili kwenye kundi D na kukata tiketi ya robo fainali.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad