KIPA wa Yanga Djigui Diarra ameipeleka Yanga, nusu fainali huku kocha wao Nasreddine Nabi akionyeshwa kadi nyekundu kutokana na utovu wa nidhamu aliouonyesha.
Diarra baada ya kukosa penati yake ya saba kwa upande wa Yanga alisawazishaakosa kwa kuokoa mkwaju wa penati uliochongwa na Maka Edward.
Yanga wamepata penati saba kati ya nane walizopiga huku Geita Gold wao wakikosa mbili na pata sita.
Penalti za Yanga zilichongwa na Yanick Bangala, Jesus Moloko, Fiston Mayele, Said Ntibazonkiza, Shaban Djuma, Bakari Mwamnyeto, Diarra alikosa na Diskson Job ambaye alipga ya ushindi.
Wakati Geita Gold wapigaji walikuwa ni Duchu, George Mpole, Maka Edward ambaye alikosa, Adeyum Saleh, Chikola, Kelvin Yondani, Juma Mahadh ambaye alikosa pia.
Hatua ya upigaji penati ilifikiwa baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 kwa sare ya bao 1-1 mabao yakifungwa na Chikola kwa upande wa Geita Gold na la Yanga lilifungwa na Shaban kwa mkwaju wa penati.
Kipindi cha pili mpira ulichezwa kwa kukamiana zaidi kipindi cha pili huku kila timu ikihitaji matokeo.
Geita Gold ndio walikuw wa kwanza kuliandama lango la Yanga baada ya Mpole kuanza kwa kupiga kichwa kilichozaa kona baada ya Diara kuokoa kona yao haikuwa na mazara.
Yanga walijibu mapigo dakika 47 na 48 kwa kupiga kona doto baada ya mabeki wa Geita Gold kuokoa mipira iliyokuwa inaelekezwa langoni mwao.
Timu zote zilifanya mabadiliko kwa muda tofauti tofauti Yanga wakianza dakik ya 50 ilimtoa Kaseke na Farid nafasi zao zilichukuliwa na Jesus Moloko na Chrispin Ngushi.
Kwa upande wa Geita dakika 69 Adeyum Saleh kaingia Jofrey Manyac na alitoka Hafidh Musda nafasi yake ilichukuliwa na Often Chikola dakika ya 79 alitoka Mauya akaingia Makambo, Dakika ya 80 alitoka Lyanga nafasi yake ilichukuliwa na Juma Mahadh