Zaidi ya Vibanda 30 Vimeteketea Katika Soko la Kurume


Zaidi ya vibanda 30 vimeteketea katika Soko la Kurume wilayani Ilala, mkoani Dar es Salaam baada ya moto kuunguza vibanda hivyo pamoja na baadhi ya maduka ya wafanyabiashara wa mabegi yaliyopo pembeni mwa jengo la Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Afajiri ya leo Aprili 8, 2022.

Moto huo unadaiwa kusababishwa na hitilafu ya umeme, lakini hadi moto huo unadhibitiwa, hakuna madhara kwa binadamu yaliyoripotiwa kutokea.

Itakumbukwa, Januari 16, 2022 Soko la Karume maarufu kama 'mchikichini' lililopo upande wa pili wa mabanda hayo yaliyoteketea leo, liliteketea moto na kuharibu mali mbalimbali za wafanyabiashara lakini wki moja baadaye wafanyabiashara waliruhusiwa kuendelea na biashara zao kama kawaida.

Katika eneo hilo kwa sasa, wapo wafanyabiashara wakiendelea na juhudi za kuondoa baadhi ya mabaki ya bidhaa zao, yakiwemo mabati na mabegi yaliyoteketea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad