ZUCHU "Nimekumiss Diamond Platnumz Rudi Bongo"


ZUCHU ni malkia mpya wa muziki nchini Tanzania ambaye kumekuwa na tetesi za miezi kadhaa sasa kwamba anatoka kimapenzi na bosi wake, Diamond Platnumz.


Sasa, taarifa ikufikie kwamba, mrembo huyo ameshindwa kuficha hisia zake kwa Diamond au Mondi wakati huu ambapo jamaa huyo yupo nchini Uingereza na barani Ulaya kwa ajili ya kutangaza albam yake fupi (EP) ya FOA.


Zuchu amefanya mazungumzo ya moja kwa moja (kwenda live) kupitia Mtandao wa Snapchat na Diamond akiwa kitandani nchini Uingereza, naye akiwa kitandani Bongo na kumueleza namna ambavyo amemmisi huku akiomba arudi nchini huku akitaka kutokwa machozi.


Diamond na Zuchu wamekuwa wakitrendi kwa miezi mitatu sasa ambapo wakiwa pamoja nchini huwa hawapoi kwani habari zaao huwa ni nyingi mno.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad