Watu wanane wamepoteza maisha katika ajali mbaya ya barabarani iliyotokea mapema leo kwenye barabara kuu ya Mai Mahiu
Ajali hiyo inaripotiwa kutokea baada ya dereva wa basi kushikwa na usingizi na kupoteza udhibiti wa gari kabla ya kugonga nan a lori la kusafirisha changarawe
Miongoni mwa waliofariki ni wanawake wanne na wanaume wanne wanaosemekana kuwa safarini kuelekea katika hafla ya mazishi Kisii
Watu wanane wameangamia katika ajali ya barabarani iliyotokea kwenye barabara ya Nairobi kuelekea Mai Mahiu asubuhi ya Jumamosi, Mei 21.
Abiria Wanane Waangamia Katika Ajali Baada ya Dereva wa Basi Kushikwa na Usingizi
Watu wanane wamepoteza maisha yao katika ajali ya barabarani Jumamosi. Picha: Citizen Digital.
Ajali hiyo iliyotokea mwendo wa saa nane usiku ilihusisha basi la abiria na gari jingine aina ya lori na kuacha watu wengine kadhaa wakiuguza majeraha.
Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, ajali hiyo ilitokea baada ya basi hilo kugonga lori lilokuwa likisafirisha changarawe kuelekea Nairobi.
Mtandao wa Citizen Digital unaripoti kuwa afisa wa polisi ambaye alikuwa eneo la tukio ajali hiyo ikitokea lakini alikataa kutajwa, anadai kuwa dereva wa basi alishikwa na usingizi akiwa kwenye usukani, basi hilo likipoteza mwelekeo na kugongana ana kwa ana na lori lililokuwa likija.
Kasri la Baba: Mbili Tatu Kuhusu Jumba la Kifahari la Raila Katika Eneo la Riat Hills
Inaarifiwa miongoni mwa waliofariki ni watu wanane, wanawake wanne na wanaume wanne, wanaosemekana kuwa katika safari ya kuelekea Kisii kwa ajili ya hafla ya maziko.
Ajali hiyo ya saa nane usiku ilisababisha msongamano mkubwa wa magari kwenye barabara kuu ya Mai Mahiu Nairobi, polisi wakilazimika kujitokeza kwa wingi ili kurejesha hali ya kawaida.
Majeruhi walikimbizwa hadi Hospitali ya Naivasha Level 4 kwa matibabu huku miili ya walioaga ikihifadhiwa katika makafani ya hospitali hiyo.