Ahmed Ally: Namungo FC watavuta PUMZI ya MOTO



Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wamesea wanatarajia mchezo wenye ushindani dhidi ya Namungo FC kesho Jumanne (Mei 03), katika Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.


Simba SC iliyotoka kuambulia matokeo ya sare ya bila kufungana dhidi ya Young Africans, imetoa mtazamo huo kupitia Meneja wa Habari na Mawasilino Ahmed Ally alipozungumza na Vyombo vya Habari mjini Mtwara, ambako wameweka kambi ya muda baada ya kuwasili mapema hii leo wakitokea jijini Dar es salaam.


Ahmed amesema Namungo FC siku zote imekua ikiwapa upinzani wa kutosha Simba SC na wanaamini hilo litatokea kwenye mchezo wa kesho, kutokana na mwenendo wa wapinznai wao katika michezo yao ya hivi karibuni.


“Namungo FC ni miongoni mwa timu zinazotupa upinzani wa kweli kwa sababu inacheza soka la ushindani, hivyo tunatarajia mchezo utakua mgumu, licha ya Simba SC kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya kuondoka na alama tatu.”


“Namungo FC ina wachezaji wenye kushindana, ina wachezaji wenye uzoefu wa Ligi, lakini niwahakikishie mashabiki wa Simba SC sisi huwa tunazitaka mechi kama hizi, ili tukishinda tuwe tumeshindwa kwa ushindani wa kweli.”


“Namungo haijawahi kutufunga sisi Simba SC, wamechezea vipigo mfululizo tangu walipopanda daraja, pia Namungo FC hii imewahi kushuhudia tukikabidhiwa Kombe la Ubingwa kwenye Uwanja wake wa nyumbani, pia ikashuhudia tukifanywa hivyo msimu uliopita Uwanja wa Mkapa, na kule Sumbawanga ilishuhudia tukifanya hivyo kwenye Fainali ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.” amesema Ahmed Ally


Simba SC ipo nafasi ya pili katika Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 42, huku ikiachwa kwa tofauti ya alama 13 dhidi ya vinara Young Africans yenye alama 55.


Namungo FC inashika nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 29 sawa na Azam FC inayoshika nafasi ya nne, kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad