Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Namungo vs Simba"


Mambo 10 nilioyaona Namungo vs Simba

1: Classic Match.. Dakika 90 zenye Mabao 4 🙌 Kwa mara ya kwanza kwenye Ligi msimu huu, Simba wanaruhusu Mabao 2 kwenye wavu wao. Kwanini?

2: 'Kisaikolojia' ni kama Simba wameshakubali mbio za Ubingwa msimu huu zimeshamalizika. 'Tactically' wakawa na mchezo wa wazi.. Na kwa 'Quality' ya kikosi cha Namungo, hasira zao za kuisaka 'Top 4' ungetegemea dakika 90 zenye mabao ya kutosha

3: Pablo Franco yuko kwenye jaribu kubwa kwenye career yake ndani ya Simba. Kivipi? Ishu sio Simba kukosa Ubingwa.. Ishu ni jinsi Simba watakavyomaliza msimu. Mabadiliko ya kikosi mara kwa mara ni changamoto anayotakiwa kujiandaa nayo kwenye uwanja wa mazoezi kuelekea mechi za mwisho

4: Kipa wa Namungo, David Mapigano Kisu✊ Simba wamefunga bao 2 lakini Ameokoa Shots On Target 7 langoni mwake. Ni mikono yake ndio iliwaweka Namungo mchezoni Simba walipopeleka presha kubwa langoni mwao

5: Kama kuna funzo Kapombe ameliacha kwenye benchi la Ufundi la Namungo ni jinsi gani 'Movement' za Masawe kama Half Spaces Midfielder zinazompa wakati mgumu beki wake wa kushoto.. Kwanini?

6: Jacob Masawe akiingia ndani, Lusajo anatakiwa kutoa pembeni. Wakiwa na mpira ni 'mpango mzuri' Lakini mpinzani anapofanya Transition ya haraka kwenda kushambulia, Beki wa kulia anachomoa akiwa Free.. Ni kujiweka kitanzi kumruhusu Kapombe awe na safari za namna ile.. What A Perfomance✊

7: Refa Omari Mdoe ni kama alipania sana. Mechi haikuendana na presha yake. 'mapepe' yalikuwa mengi kiasi cha kukosa umakini kwenye baadhi ya maamuzi yake

8: Molinga.. Yes, alijaribu kuwa bora kwenye kumiliki mpira Lakini inahitaji maelezo mengi sana kuona 'impact' yake inayostahili kuwa kwenye kikosi cha kwanza mbele ya Obrey Chirwa! Bado inahitaji 'Details' nyingi za kiufundi kuelewa hili

9: Nilipenda Battle ya Muzamir na Kitanta pale katikati✊ Tunapozungumza kuhusu upambanaji wa Masawe tusisahau kuelezea ubora wa ile pasi ya Muzamir kwa Kapombe..🙌

10: Kama viongozi wa Simba wanafikiri msimu uliopita walifanya Usajili mkubwa.. basi wafikirie tena. Hizi mechi za mwisho hapa zitawapa majibu juu ya Tofauti ya 'quality' ya ubora kwenye kikosi chao

Nb: Kubwa lakini haliwashi tena😃

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad