Aliyeamua fainali Simba, Yanga Kigoma, apewa nusu fainali Kirumba



MWAMUZI Ahmed Arajiga ndiye alieyepewa kuchezesha mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam baina ya Yanga na Simba, Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Uamuzi wa kumteua Arajiga umetokana na Ramadhan Kayoko ambaye alikuwa anapewa nafasi kubwa hapo awali, kuwa tayari ameshachezesha mechi iliyopita ya Yanga na Simba katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu msimu huu ambayo uliomalizika kwa sare tasa.

Arajiga anakumbukwa vyema kwa kuchezesha mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam mwaka jana baina ya timu hizo mbili kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma ambayo Simba waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Lwanga Taddeo.

Hivi karibuni refa huyo alichezesha mechi ya Ligi Kuu baina ya Geita Gold na Simba iliyochezwa katika Uwanja huohuo wa CCM Kirumba ambayo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1.


 
Arajiga alipewa beji ya Fifa kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa mwaka huu na kumfanya kuwa miongoni mwa marefa wa tatu tu wa kati wa kiume ambao nao wana beji za kimataifa za uamuzi wa soka.

Mwamuzi huyo aliyechezesha mechi ya nusu fainali ya Kombe hilo kati Azam FC na Simba msimu uliopita kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea na kuamua mchezo wa fainali kati ya Simba vs Yanga uliochezwa Julai 25 mwaka jana kwenye Dimba la Lake Tanganyika, Kigoma.

Wakati Arajiga akipewa nafasi hiyo ya Jumamosi, marefa watatu wasaidizi ni Mohamed Mkono, Elly Sasii na Frank Komba.

Katika dimba la Sheikh Amri Abeid, mwamuzi Ramadhan Kayoko ataamua mechi ya Coastal Union dhidi ya Azam FC Jumapili Mei 29.

KAMBI ZANOGA

Simba na Yanga wote wapo Kanda ya Ziwa, lakini Yanga baada ya mechi yao na Biashara iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1 walisafiri hadi Shinyanga kwa ajili ya kambi huku Simba wakibaki Isamilo, Mwanza na mazoezi yao wanafanyia Uwanja wa Gwambina uliopo Misungwi.

Tayari asilimia kubwa ya vigogo wa timu hizo wako kambini kuweka mambo sawa mtu apigwe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad