Ang'atwa na Nyoka Makalioni Wakati Akijisaidia Kwenye Choo Cha Kukalia



Jamaa huyo kwa jina Sabri Tazal(28) amepatwa na mshtuko wa aina yake baada ya kung'atwa na nyoka katika kalio wakati akiwa anajisaidia haja kubwa katika choo cha kukaa huku anacheza game katika simu yake

Tukio limetokea nchini Malaysia nyumbani kwa jamaa huyo. Hata havyo, bahati yake nyoka huyo(python) hakuwa na sumu ila aliacha kipande cha jino kwenye kalio la jamaa wakati alipomtoa kwa nguvu na kumbamiza ukutani baada ya kusikia kung'atwa


Jamaa alipatwa na paniki hadi kuvunja mlango wa chooni kwake wakati akitaka kuufungua achomoke mbio kujinusuru. Firefighters walifika baada ya muda na kumtoa nyoka husika

Ingawa nyoka huyo(python) hana sumu lakini jamaa alifika hospitali ya karibu akaangaliwa jeraha husika na kupewa huduma ya kitabibu ya kumkinga/kupambana na tetenasi

Akihojiwa na waandishi amesema tukio hilo bado limemkoroga afya yake ya akili kiasi cha kushindwa tena kujisaidia chooni kwake kwa wiki mbili sasa na badala yake amekuwa akienda kujisadia katika msikiti uliopo karibu


Anyway, ukiacha matukio mengi ya watu kung'atwa na nyoka vyooni kutokea zaidi katika vyoo vya kukaa, ila mimi binafsi sijawahi kuvutiwa kabisa kutumia hivi vyoo vya kukaa sababu zikiwa masuala ya kiusafi, yaani ile kila mtu anakuja anakaa hata choo kiwe kisafi mimi mood huwa inanitoka unatamani bora kwenda choo cha shimo kisicho na sink 😂 sijawahi kuvutiwa navyo kabisa hata kama nikitumie peke yangu. Kama ndio usasa bora nionekane mshamba ila choo kiwe cha sink la kawaida sio la sink la kukaa

Nakumbuka chuo nilichosoma wachina walivijenga vingi wanafunzi walipoanza kuvitumia hali ikawa tete katika masuala haya haya ya usafi na shida ya maji iliyokuwepo Dodoma walianza kubomoa wakaweka masink ya kawaida

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mimi kwa kuwa ni Mzee napenda sana vyoo vya kukalia. Ninyi ambao bado mnaweza kukunja miguu, mnapenda vyoo vya Asia vya kuchuvhumaa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad