Askofu Ruwa’ichi kutoa tamko mtawa anayedaiwa utapeli



Dodoma. Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi anatarajia kutoa tamko juu ya sintofahamu ya mtawa ambaye anadaiwa kuwa tapeli.

Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii ilichapishwa picha ya mwanamke aliyevalia mavazi ya kitawa na kuambatana na maelezo kuwa, Dekano wa Dekania ya Mbezi Luis ametahadharisha watu kuwa makini na mtawa huyo na kwamba ni tapeli.

Hata hivyo, familia ya mtawa Martha Mwasu na viongozi wa Kanisa walikutana juzi kujadili suala hilo kiimani ambapo mtuhumiwa (Dekania) aliomba msamaha kwa kuchapisha maudhui hayo bila kujiridhisha.

Akizungumza na Mwananchi, Peter Jimbuka, baba mdogo wa mtawa huyo alisema kuwa kutokana na jambo hilo limefika ngazi za juu za uongozi wa kikanisa, Askofu Mkuu Ruwa’ichi atatolea maamuzi Mei 30, 2022, baada ya kufanyika kwa kikao hicho


 
“Maamuzi na matamko yote ya Kanisa hutolewa na yeye, Jumatatu amesema atalitolea tamko lakini juzi tulikutana na mtuhumiwa aliomba radhi kwa kuchapisha maudhui hayo bila kujiridhisha,” alisema.

Ilivyokuwa

Mei 14, 2022 Martha Mwasu alisafiri kutoka mkoani Morogoro kwenda jijini Dar es Salaam akiwa na timu ya watawa wengine kuhudhuria sherehe za Upadirisho katika Parokia ya Mtoni.

Pater anasimulia kuwa baadaye Martha aliwataarifu wenzake kuwa hataambatana nao kurudi Morogoro, badala yake atabaki kufuatilia mambo yake binafsi ikiwemo ushahidi wa mvutano uliopo kati yake na aliyempa kiwanja mkoani Morogoro.


“Baada ya kumaliza sherehe ilikuwa jioni sana, hivyo alipanda gari ya redio Maria na ilimshusha Mwenge ambapo baada ya kufika hapo hakuwakuta watu aliopanga kukutana nao na tayari usiku uliingia, alipanda gari hadi Mbezi akiwa na lengo la kuja nyumbani kwangu,” alisema.

Peter alisema baada ya mtawa huyo kufika kituoni Mbezi alishindwa kuwasiliana naye kwa kuwa simu ya mtawa huyo ilizima chaji na alikuwa hapajui anapoenda.

Alisema baada ya kukosa mwelekeo na usiku kuzidi, aliomba kuoneshwa mahali kanisa lilipo na alisindikizwa na kijana mmoja kwa ajili ya usalama wa muda huo.

Alisema baada ya kufika kanisani hapo aliwaomba walinzi kukutana na padri kwa ajili ya kumuomba hifadhi ya kulala ili asubuhi aamkie kwa baba yake mdogo. Lakini walimtoa nje


 
Alisema baada ya kutolewa nje ilipita familia iliyokuwa inatoka kwenye sherehe na kumuuliza nini kilichomfanya awe nje na kumpatia msaada wa bajaji ambayo ilimpeleka kwenye nyumba za watawa zilizopo Mbezi Uluguruni.

Baada ya kufika getini walinzi na watawa wawili walimhoji na kuonesha kutoridhishwa na maelezo yake, lakini walimsaidia kwa kumlaza kwenye wodi moja kwenye hospitali hiyo ya masista.

“Asubuhi aliamkia kanisani kwa ajili ya ibada na baada ya kuomba chaji alipata mawasiliano na kuanza safari ya kuja nyumbani kwangu, na alifika salama” alisema.

Peter alisema Jumatatu asubuhi aliongozana naye kwa ajili ya kumuonesha vituo na alimuomba konda amshushe kituo cha Bamaga akiwa na lengo la kukutana na watu (mashahidi) aliopanga kukutana nao.


Baada ya kufika kituoni akiwa na lengo la kutafuta mgahawa kwa ajili ya kunywa chai alimuona mtawa mwenzake ambaye aliona kuwa atamsaidia kumuonesha mgahawa.

“Cha kushangaza baada ya kusalimiana yule mtawa alimuuliza, “Umelala wapi na unakwenda wapi? Kabla hajamjibu alichukua simu yake na kumpiga picha kisha kuondoka zake,” alisema
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad