Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imefanya maboresho ya Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22.
TPLB imefanya mabadiliko hayo saa chache baada ya Shirikisho la Soka nchini Tanzania kutoa Ratiba ya michezo ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ ambayo itachezwa Jumamosi (Mei 28) na Jumapili (Mei 29).
Mabadiliko hayo yamegusa muda wa kuanza kwa michezo husika, pamoja na kusogezwa mbele ama kurudishwa nyuma kwa siku moja kwa michezo hiyo.
Taarfa iliyotolewa na TPLB na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii imeonyesha, Michezo iliyofanyiwa mabadiliko ni kama ifuatavyo:
Mechi na. 189 Polisi Tanzania FC dhidi ya Biashara United FC itachezwa Mei 30, 2022 saa kumi (10:00) kamili jioni katika uwanja wa ushirika uliopo Kilimanjaro badala ya Mei 21, 2022 saa nane (8:00) kamili mchana kama ilivyokuwa awali
Mechi na. 191 Young Africans SC dhidi ya Mbeya Kwanza FC itachezwa mei 20, 2022 saa moja (1:00) kamili usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam badala ya Mei 21, 2022 kama ilivyokuwa awali.
Mechi na. 196, Biashara United FC dhidi ya Young Africans SC itachezwa Mei 23, 2022 saa kumi (10:00) kamili jioni katika uwanja wa CCM Kirumba uliopo Mwanza badala ya Mei 24, 2022 kama ilivyokuwa awali.
Mechi na. 199 Simba SC dhidi ya KMC FC itachezwa Juni 19, 2022 saa moja (1:00) kamili usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam badala ya Mei 25, 2022 kama ilivyokuwa awali.
Mechi na. 223 KMC FC dhidi ya Mbeya Kwanza FC itachezwa Juni 22, 2022 saa kumi (10:00) kamili jioni katika uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam badala ya Juni 21, 2022 kama ilivyokuwa awali.
Sababu za maboresho haya ni:
Kupisha ratiba ya mechi za timu ya taifa (CAF AFCON 2023 QUALIFIERS).
Kupisha ratiba ya michezo ya kombe la shirikisho (ASFC) hatua ya nusu fainali.
Kuwahi tarehe ya kupeleka majina CAF Juni 30, 2022.
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) inakutakia maandalizi mema ya michezo uliyonayo.