Breaking News : Mishahara Mbioni Kupanda, Majaliwa Apokea Pendekezo

 


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amepokea taarifa ya mapendekezo ya ongezeko la mishahara ya watumishi kutoka kwa timu ya wataalamu iliyokuwa ikiyaandaa kwa ajili ya kuiwasilisha kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amepokea taarifa hiyo leo usiku (Jumanne, Mei 10, 2022) katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.

Kikao hicho kiliwahusisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Viongozi wengine waliohudhuria kikao hicho ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi pamoja na Makatibu Wakuu wa wizara hizo.

Mheshimiwa Majaliwa amesema taarifa hiyo imeonesha kwamba maandalizi ya mapendekezo ya ongezeko la mishahara yameshakamilika na kwamba wakati wowote atayawasilisha kwa Mheshimiwa Rais Samia ambaye atautangazia umma mabadiliko hayo yanayotarajiwa Julai mwaka huu.

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia wananchi katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Jumapili Mei Mosi 2022 aliwahikikishia wafanyakazi nchini kuwa Serikali katika mwaka wa fedha 2022/2023 itaongeza mishahara kwa watumishi wake.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad