Dar es Salaam. Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi imemsimamisha Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia na makamu Mwenyekiti Bara, Angelina Mtahiwa kutojihusisha na shuhhuli zozote za chama hadi mkutano Mkuu utakapoitishwa ili wajieleze kuhusiana na tuhuma inazowakubali.
Uwamuzi huo umefanyika leo Jumamosi Mei 21, 2022 kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kugombanisha viongozi na kulazimisha kujiuzulu.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mwenyekiti wa azimio hilo, Joseph Selasini amesema pamoja na kusimamishwa kwa viongozi hao pia wamelivunja Baraza la Wadhamini la NCCR na kuteua wajumbe wapya ambao watasajiliwa kwa mujibu wa taratibu zitakazowekwa.
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Sisty Nyahoza amesema walipokea barua kutoka NCCR-Mageuzi kuwa kuna mabadiliko ya wajumbe wa bodi ya wadhamini.
Amesema pamoja na mabadiliko hayo kulikuwa na ajenda nyingine ambayo ni kusimamishwa kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Bara kutokana na maazimio hayo wanasubiri barua rasmi ili kutoa taarifa.
"Tuna orodha yetu tutaenda kuangalia kama mlivyoona wajumbe wapo na akidi imetimia hivyo tunangoja barua rasmi kisha tutaenda kupitia na katiba yao," amesema Nyahoza