MKUTANO wa saba kikao cha 16 cha Bunge la Tanzania leo Alhamisi kumesimamisha shughuli zake za kawaida na kuanza kujadili kupanda kwa bei za mafuta. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Ni baada ya Mbunge wa Kilindi (CCM) kutoa hoja ya kuahirisha shughuli za Bunge na kujadili suala la kupanda bei ya mafuta ambapo imefikia zaidi ya Sh.3,000 kwa mafuta ya petrol na dizel.
Baada ya kutoa hoja hiyo, Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameirihusu na wabunge wanachangia na kutoa ushauri wa nini cha kufanya.