CAF yairahisishia kibarua Stars CHAN



Taifa Stars imeshiriki Fainali za CHAN mara mbili ambapo ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2009 na nyingine ikawa ni 2021.
stars pic
Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imeandaliwa mazingira mazuri ya kufuzu fainali zijazo za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuongeza idadi ya timu shiriki kutoka 16.

Uamuzi wa kuongeza idadi ya timu katika mashindano hayo umefanywa na kamati ya utendaji ya CAF iliyoketi hivi karibuni huko Cairo, Misri.

Taarifa iliyotumwa na mkurugenzi wa mashindano wa CAF, Samson Adam kwenda kwa mashirikisho na vyama vya soka vya nchi wanachama wa shirikisho hilo, imefafanua nyongeza ya idadi ya timu za kufuzu mashindano hayo kwa kila kanda ya soka.

"Tunakujulisha kwamba kamati ya utendaji ya CAF imepitisha ongezeko la timu kwenye awamu ijayo ya mashindano ya CHAN hadi timu 18," ilifafanua sehemu ya taarifa hiyo ya CAF.


 
Kwa mujibu wa ongezeko hilo, kila kanda iliyo chini ya CAF itawakilishwa na timu tatu katika mashindano hayo yatakayofanyika mwakani huko Algeria.

Kwa ongezeko hilo, Kanda ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) itawakilishwa na timu tatu badala ya mbili kama ilivyokuwa hapo awali.

Awamu iliyopita mashindano hayo yalipofanyika Cameroon, CECAFA iliwakilishwa na Taifa Stars na Uganda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad