Colombia jana Alhamis, limekuwa taifa la kwanza katika eneo la kusini mwa Amerika kutoa idhini ya mgonjwa kusaidiwa kujiua kwa sababu za kitabibu, akiwa chini ya uangalizi wa daktari.
Hatua hiyo ni kwa mujibu wa mahakama ya kikatiba ya taifa hilo. Mahakama imetoa uamuzi kwamba daktari anaweza kumsaidia mgonjwa mahututi kujiua kwa kutumia dawa ya sumu, bila ya daktari huyo kuwa katika hatari ya kufungwa.
Hata hivyo Colombia ilikuwa tayari imetoa aina fulani ya ruhusa ya mgonjwa kujitoa uhai ambapo daktari aliweza kumpa mgonjwa husika dawa ya kulitekeleza hilo.