Edo Kumwembe "Watanzania Tunaumwa, Tuna Matatizo ya Akili Tunatembea Nayo Huku Tumevaa Nguo"



From Edo kumwembe

"Tunaumwa tunaumwa tunaumwa...jamaa mmoja alihamia mtaani kwetu...alikuwa mkimya sana. Alipenda kujichanganya na sisi lakini alikuwa haongei kabisa. Alikuwa mkimya mno. Siku moja mtaani kwetu akapigwa mwizi. Huyu jamaa mkimya Ila kitu alichokwenda kumfanya mwizi wote hatukuamini. Tulianza kumuogopa tangu siku. Alimkata mwizi vidole, akataka kumtoboa macho. Wote tulikimbia.

Baadaye nikagundua ukimya wa huyu jamaa haukuwa wa bure. Alikuwa anahifadhi vitu vingi moyoni. Na kwa kiasi kikubwa alikuwa na matatizo ya kisaikolojia. Watanzania tunaumwa. Huyu aliyeua Mwanza akili yake ilikuwa inaumwa. Kabla ya hapo nimesikia kuna mtoto wa miezi sita amelawatiwa mahala. kuna yule aliyembaka Mama yake. Kuna huyu Mama aliyemnyonga mwanae..

Watanzania tunaumwa. Tuna matatizo ya akili tunatembea nayo huku tukiwa tumevaa nguo nzuri, tunaendesha magari mazuri, tunakaa nyumba nzuri lakini akili zetu zinaumwa. Nchi yetu haina wataalamu wa Saikolojia. Mama zetu na Dada zetu huwa wanakimbilia kwa Wachungaji hasa wanapotingwa na issue za kukosa watoto na mengineyo. Tatizo kuna wachungaji feki wanaofanya waumwe zaidi.. Sisi wengine tunaumwa na tunasubiri kufanya jambo lolote la hatari kwa sababu hatuna mtu wa kutusaidia tusifikirie tunayoyafikiria. Haijalishi wenye pesa au maskini...

Watanzania wengi wana msongo wa mawazo....mental sickness ni ugonjwa mbaya ambao unatumaliza kimya kimya sisi tupo busy zaidi na Malaria, HIV, vidonda vya tumbo...sio mbaya lakini tuungalie na ugonjwa huu unaotumaliza....' LEGEND

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad