Nchini Kenya, kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi agosti mwaka huu, wanasiasa kwenye taifa hilo la Afrika mashariki wanaendelea kufanya kampeni za kuwaraia wapiga kura kuwachagua katika wakati wa uchaguzi huo.
Maneno makali yamekuwa yakishuhudia kati ya naibu wa rais William Ruto na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga wote wanaotaka kumrithi rais Kenyatta anayemaliza hatamu yake ya kuongoza taifa hilo baada ya miaka 10.
William Ruto anayewania kupitia mrengo wa Kenya kwanza, amemtaka Raila Odinga, ambaye anawania urais kwa tiketi ya Azimio la umoja kustaafu na kwenda na kuwachana na siasa.
Ruto, akiwa katika harakati zake za kutafuta uungwaji mkono magharibi ya Kenya, eneo ambalo kwa muda sasa limeonekana kuwa ngome ya Raila, amesema kuwa Odinga hana uwezo wa kutekeleza jambo lolote njema kwa raia wa taifa la Kenya na hawezi maliza ufisadi.
Ruto aidha ameendelea kukashifu maafikiano kati ya rais Kenyatta na Odinga maarufu kama Handshake, hatua anayosema imechangia pakubwa uwepo wa mianya ya ufisadi nchini Kenya.
Naibu huyo wa rais vilevile ametaka Odinga kuwajibikia kupotea kwa fedha kwenye shirika la usambazaji dawa nchini humo KEMSA.
Mwezi jana, Raila aliahidi kuwa atamaliza ufisadi iwapo wakenya watamchagua katika kura za urais za agosti tisa akieleza kuguswa na jinamizi la ufisadi nchini humo.
Odinga ameendelea kusisitiza mpango wake wa kuwapa wakenya wote wasio na ajira shillingi elfu sita pesa za kenya unawezekana na anajuwa mahali pesa za kufanya hivyo zipo.
Kinara huo wa chama ODM kwa mara kadhaa katika vyombo vya habari na mikutano ya kampeni amekuwa akimtaja naibu rais William Ruto kama mtu asiwezakuelezea vyanzo vya utajiri wake.