French Montana kufikishwa Mahakamani kwa kesi ya wizi


French Montana pengine akaburuzwa mahakamani hivi karibuni kufuatia kushutumiwa kuiba mashairi ya wimbo wa kundi maarufu la Hip Hop la muda mrefu ‘Hot Boys’.


Rapa Turk ambaye ni mmoja wa wahusika wa kundi hilo anadai French anapaswa kushughulikia suala la kutafuta suluhu hivi karibuni kabla ya kesi hiyo kwenda mbali zaidi.


Rapa Turk ambaye jina lake kamili ni Tab Virgil Jr, amewataka mawakili wake kufuatilia barua ya madai kwa wakili wa French Montana, kwa madai ya French kunakili baadhi ya mashairi kutoka kwenye wimbo a mteja wao na kuhamishia kwenye wimbo wake ‘Handstand’ alioutoa mapema mwaka 2021.


Kwa mujibu wa barua hiyo iliyopatikana na TMZ inìadai kuwa Montana alijibebea mashairi kutoka kwa wimbo wa kundi hilo wa mwaka 1999 uitwao “I Need A Hot Girl” bila ya makubaliano wala kupata kibali cha idhini ya matumizi ya mashairi hayo, na kuongeza kuwa wimbo aliounakili Montana mpaka sasa una jumla ya watazamaji zaidi ya milioni 17 kwenye mtandao wa YouTube, mafanikio yanayotokana na wimbo wenye mashairi ya wizi.


Kwa upande mwingine wakili wa Turk, Paul M. Aloise anaungana na ushauri wa rapa huyo wakimtaka Montana kuwajibika kutafuta suluhu mapema kwa kuwa wao wako tayari kusuluhishwa kesi hiyo nje ya mahakama, hivyo ikiwa French Montana atafuata ushauri huo, yapo matumaini kuwa kesi hiyo itatuliwa hivi karibuni.


Kama hukuwahi kufahamu, Kundi la ‘The Hot Boys’ ni moja ya makundi bora ya muziki wa hip hop lililoanzishwa mwanzoni mwa miaka ya 90 na wanachama (Member’s) wa kundi hilo walikuwa rapa Lil Wayne, B.G, juvenile, pamoja na rap Turk ambaye ndiye mwenye kusimamia kesi hiyo.


Wimbo huo ambao Montana amenakili mashairi yake uitwao “I Need A Hot Girl”, ulifanikiwa kufanya vizuri na kuvuma sana wakati huo kiasi cha kuchumpa mpaka nafasi za juu kwenye chati Billboards Hot 100.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad