Halima Mdee, wenzake hawapo bungeni



By Habel Chidawali
Dodoma. Wabunge 19 wa Viti Maalumu wa Chedema leo hawajaonekana bungeni katika upande wanapokaa huku viti vyao vikwa wazi.

 Kundi hilo maarufu Halima Mdee na wenzake jana walikuwa bungeni na baadhi yao walipata nafasi ya kuuliza maswali na kuchangia makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka 2022/2023..

Wabunge hao ambao hukaa mbele pembeni kushoto mwa kiti cha Spika hawakuonekana muda wote wa kipindi cha maswali na majibu na walioonekana kwa upande huo walikuwa ni wabunge wa ACT-Wazalendo ambao nao hukaa upande huo.

Kulikuwa na taarifa za wabunge wa Chadema kuitwa kwenye kikao cha Baraza Kuu la Chadema ambacho kinafanyika leo jijini Dar es Salaam ambako wanaitwa kwenda kuhojiwa kuhusu uteuzi wao wa kuingia bungeni.


 
Wabunge hao wamekuwa na mgogoro na chama chao ambacho Novemba 27, 2020 kiliwaandikia barua ya kuwatimua kwenye chama ndipo wakakata rufaa Baraza Kuu.

Juzi zilisambaa taarifa bungeni kuwa wabunge hao hawatakuwa bungeni kwani watahitaji kwenda kutetea nafasi zao huko huku baadhi yao wakionyesha kujiamini kuwa wanaweza kuvuka kihunzi hicho na kurejea tena bungeni.

Kama watashindwa kutetea rufaa yao huenda mkutano huu ukawa ni wa mwisho kwao kushiriki vikao vya bunge na hivyo kutakuwa na uapishaji wa wabunge wengine wapya kabla ya kuhitimishwa kwa mkutano huu ambao utamaliza shughuli zake Juni 30, 2022.

Leo Chadema kinafanya kikao cha baraza kuu litakalokuwa ajenda tano na kuhudhuria na wajumbe zaidi ya 400 wa chama hicho, watakaotoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema Baraza Kuu litakuwa na ajenda tano ambayo ni mpango mkakati wa chama kwa miaka tano pamoja na mpango kazi wa mwaka.

Mrema alisema sema ajenda nyingine itakuwa ni rufaa ya nidhamu iliyokatwa na wabunge 19 wa viti maalumu wakiongozwa na Halima Mdee wakipinga kuvuliwa uanachama na kamati kuu ya chama hicho iliyoketi mwisho mwa mwaka 2020.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad