HISIA ZANGU: Nani alimfundisha George Mpole kuongea vizuri?



NILIKUWA namsikiliza George Mpole mahala. Mshambuliaji mahiri wa Geita Gold ya Ligi Kuu. Alikuwa akihojiwa na waandishi wa habari. Swali lilikuwa kuhusu mbio zake za kuwania kiatu cha ufungaji bora wa Ligi Kuu na mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele. Alinikosha.

“Mimi sipo katika presha yoyote. Nipo kwa ajili ya kuisaidia timu. Sipo kwa ajili ya kupambana na mtu wala timu yoyote. Nipo kwa ajili ya kuisaidia timu,” alisema Mpole dakika chache baada ya kufunga bao la 14 la msimu ambalo linamfanya kuendelea kupambania kiatu cha mfungaji bora.

Kabla ya hapo alikuwa amesema: “Siwezi kuridhika. Siwezi kusema kwamba kwa sababu nina mabao 14 basi niridhike. Mechi bado na mwisho wa msimu ndio tutaangalia nimefunga mabao mangapi na kama timu imefikia malengo yake.” Nilikoshwa na maongezi ya mchezaji wa namna hii. Kwa sasa ndiye habari ya mjini. Nyuma yake anapata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wa timu yake, lakini vilevile kwa mashabiki wa watani wa Yanga, Simba ambao wanatamani Mpole awe mfungaji bora mbele ya Mayele.

Lakini kuna swali linazidi kuenea mtaani. Kwanini Mayele anasifika zaidi ya Mpole wakati mpaka sasa (kabla ya mechi za jana) Mpole anaonekana kuwa kinara wa mabao? Ukweli upo wazi kwamba Mayele anacheza katika timu kubwa ambayo ina mashabiki wengi.


 
Lakini Mayele ana staili yake ya ushangiliaji ambayo inawakosha wengi. Zaidi ya hapo staili hiyo na mabao hayo ameyapeleka katika timu ambayo ilikuwa na kiu ya kupata mshambuliaji wa aina yake. Kwa kizungu tunaweza kusema mashabiki wa Yanga walikuwa ‘desperate’ ya kuwa na mshambuliaji kama yeye.

Katika hali kama hii ya Mayele kusifiwa sana kuliko yeye, kwa ninavyowafahamu wachezaji wetu wasivyokuwa na diplomasia ya maongezi sio ajabu Mpole angeropoka vitu vingi baada ya swali linalomhusu yeye na Mayele.

Amejibu vyema. Kwanza kabisa shukrani kwake ameiongelea timu zaidi kuliko alivyojiongelea yeye mwenyewe. Ameongelea nafasi ya timu yake. Katika mchezo wa soka timu ni kitu muhimu zaidi.


Katika michezo ambayo inahusisha mchezaji mmoja mmoja, bado watu waliopo nyuma yako ni muhimu zaidi hata kama hawachezi. Kuanzia tenisi, gofu, ndondi na michezo mingine inayohusisha mchezaji mmoja mmoja, timu ni kitu muhimu zaidi. kuna watu hawalali kwa sababu yako.

Na hata katika suala la Mpole, kama ilivyo kwa Mayele na wachezaji wengine wanaofunga mabao. Huwa hawafanyi hivyo peke yao. Hata wachezaji wanaoweza kupiga chenga wachezaji saba uwanjani bado huwa wanapokea mpira kutoka kwa mchezaji mwingine. Mpole ameizungumzia timu na ni kitu muhimu.

Baada ya hapo Mpole amenikosha zaidi kwa sababu hakutaka kumzungumzia Mayele kwa ubaya. Angekuwa mchezaji mwingine angeweza kusema “Hawa kina Mayele wanabebwa tu, lakini hata sisi tunajua sana kutupia. Basi tu wanalipwa pesa nyingi lakini hawana lolote.”

Wachezaji wetu kadhaa wamewahi kusema hivyo. Hawana diplomasia pindi wanapoongea na vyombo vya habari. Sio wachezaji tu, hata makocha hasa wazawa nao hukumbwa na jinamizi hili. Hata viongozi pia huongea mbovu kwa wachezaji wa timu pinzani.


 
Mfano aliyekuwa kocha wa Tanzania Prisons, Shaaban Kazumba alivyozungumza mbovu kuhusu Yanga baada ya kumalizika kwa pambano la kwanza kati ya Yanga na Prisons pale Sumbawanga. Baadaye Kazumba alifukuzwa na timu yake kwa ubovu wa timu. Dunia huwa ina vichekesho vingi.

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anacheza nafasi ya kiungo pale Simba. Naambiwa alikuwa anajiona bora kuliko Clatous Chota Chama aliyekuwa anacheza nafasi yake. Muda mwingi alikuwa anaamini kwamba Chama na wageni walikuwa hawana vipaji vikubwa kuliko yeye.

Lakini wote tunamkumbuka Abdulhalim Humud. Baada ya pambano kati ya Tanzania na Ivory Coast kumalizika mwaka 2012 alijikuta akiwabwatukia wachezaji mastaa wa Ivory Coast. “Hawa wachezaji wa kawaida tu. Basi tu wamekwenda Ulaya lakini wana miguu kama sisi na mpira ni uleule.”

Humud alikuwa anamaanisha wachezaji kama Yaya Toure, Didier Drogba, Solomon Kalou na wengineo. Yaani mchezaji anayecheza Mtibwa Sugar anawakashifu wachezaji wanaocheza Manchester City na Chelsea. Nchi yetu haijawahi kuishiwa vioja.

Ndio maana nimempongeza Mpole. Anaweza kuwa mfano kwa wachezaji wengine wazawa katika namna ya kuzungumza na vyombo vya habari. Wakati mwingine inakusaidia kutojiweka katika hali ngumu baadaye. Kwa mfano, Mpole haijui kesho yake. Anaweza kujikuta akicheza timu moja na Mayele. Iwe Yanga au Geita Gold. Ndio maana wachezaji wengi wenye akili huwa wanaendesha mahojiano yao vyema huku wakiweka akiba ya maneno.

Hata makocha wengi wenye akili huwa wanaendesha mahojiano yao kwa akili bila ya kumuudhi mtu. Leo Kazumba anaweza kuajiriwa Yanga? Lakini hata katika hali ya kawaida Mpole anastahili heshima tu kwa Mayele na Yanga yenyewe. Kwanza kabisa licha ya kumpita Mayele kwa mabao (kabla ya jana) lakini huu ndio kwanza msimu wa kwanza kwa Mayele Yanga. Anastahili pongezi hata kama anapewa sifa zaidi yake. Lakini pia historia inaonyesha kuwa Mayele ni mshambuliaji hatari tangu alikotoka. Alipokuwa Vita alikuwa miongoni mwa wafungaji bora wa Ligi Kuu ya DR Congo. Huu ni mwendelezo tu wa ufungaji wake mzuri katika mchezo wa soka. Mpole haijui kesho yake. Anahitajika kuwa mfungaji bora tena msimu unaokuja kabla ya kujilinganisha na Mayele. Akipitisha mabao 10 kwa mara nyingine anaweza kuwa mfungaji anayenyemelea viatu vya John Bocco katika hadhi ya wafungaji wazawa katika soka.

Lakini, narudi kutoa shukrani kwa Mpole kwa sababu katika mchezo wa soka wakati mwingine mabao yanakuwa hayana maana kama malengo ya timu huwa hayafikiwi. Tumeona kilichotokea kwa Manchester United msimu huu. Cristiano Ronaldo amefunga zaidi ya mabao 20 lakini United imeshindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa. Imeangukia nafasi ya sita.

Hapohapo tumeona kuwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa pale United ni sifuri. Ina maana kwamba jitihada zote za Ronaldo zilikuwa zinakwamishwa na safu ya ulinzi. Imekuwa kazi bure. Wakati mwingine ni vizuri kuangalia nafasi ambazo Geita na Yanga zinamaliza katika msimu kuliko mabao ya Mpole na Mayele.


 

Kuwa wa kwanza kutoa maoni



Toa maoni yako

Want To Learn A Language In 2022? Expert Explains The "15 Minute" Method
Babbel
|
Sponsored
by Taboola
Unaweza kuwapenda watu
Makocha 6 ambao hawajawahi kufukuzwa


5
ippmedia.com


Inonga, Mayele siyo mchezo


34
mwanaspoti.co.tz


Kijana apigwa Risasi mbili za mguu Arusha akizuia nyumba yake isivunjwe (video+)


50
millardayo.com


RC Mtaka amuita mfanyakazi za ndani aliyefaulu


5
6h
mwananchi.co.tz


Habari mpya
Diamond Hanunui Private Jet Kwa Ajili ya Show Off , Ataja Sababu Hizi Muhimu ya Kuwa na Ndege

1h
udakuspecially.com


Namna ya kumbana Bodaboda, Bajaj, teksi kuleta hesabu


1
jamhurimedia.co.tz


Ni kilimo cha ‘kufa’ tu au ‘kufa na kupona’?

8h
jamhurimedia.co.tz


CHATI YA LATRA ILIYOCHUJUKA

5d
zanzinews.com


Get Donations from USA for Your Business in Dar Es Salaam
Donations | Search Ads
Hair Transplantion Prices Might Surprise You
Hair Transplantation
by TaboolaSponsored Links


1

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad