LONDON, ENGLAND. TAJIRI ametua. Wiki iliyopita wakati mechi ya Chelsea na Wolves inaendelea, upande wa jukwaa la VIP, kamera zilikuwa zikimuonyesha bilionea ambaye yupo kwenye hatua za mwisho za kuimiliki Chelsea Todd Boehly.
Bilionea huyu anainunua Chelsea baada ya kusubiri kwa muda mrefu mchakato wa ofa kupokelewa hadi kufikia kukubalia kuichukua timu hiyo kwa Pauni 4.25 bilioni.
Inawezekana ukawa unajiuliza jamaa amepata wapi kiasi kikubwa cha pesa kama hicho. Twende sawa uone jamaa anavyopiga pesa.
ANAPIGAJE PESA
Ana utajiri unaokadiriwa kufikia Pauni 3. 6 bilioni na hiyo haikuwa mara yake ya kwanza kuhitaji kuinunua Chelsea kwani aliwahi kujaribu suala hilo mwaka 2019 ambapo aliweka mezani ofa ya Pauni 2.2 bilioni lakini ilikataliwa.
Chanzo kikubwa cha utajiri wa jamaa ni biashara mbali mbali anazofanya, kwanza aliwahi kuwa rais wa kampuni ya Guggenheim Partners kabla ya kuachana nayo na kuunda timu ndogo ya watu ambao waliounda kampuni ya Eldridge Industries ambayo yeye anahudumu kama mtendaji mkuu na rais wa kampuni.
Kampuni hii imejikita zaidi kwenye kuwekeza kwenye sekta mbalimbali za kibiashara pamoja na michezo, pia kampuni hiyo imekuwa ikitoa mikopo.
Tajiri huyu pia anamiliki hisa za asilimia 20 kwenye timu ya Basseball Los Angeles Dodgers ambato mwaka jana iliweka rekodi yakuwa timu iliyolipa kiasi kikubwa cha pesa kwenye mishahara na kodi ambapo ilitoa Dola 285 milioni ambayo ilikuwa ni mara ya pili kufanya hivyo, mara ya kwanza ikiwa ni ile ya mwaka 2015 ambapo walikuwa na bili ya Dola 291 milioni.
Pia kampuni hii iliweka rekodi ya kuingia kwenye orodha ya makampuni yanayotoa mikopo ya mikubwa zaidi Duniani ambapo kwa upande wao imefikia Dola 1 bilioni.
Kipato cha tajiri huyu ndani ya mwaka mmoja kinakadiriwa kuwa ni zaidi ya dola 200 milioni kutoka kwa vyanzo vyake vya mapato.
Kampuni nyingine ambazo anazimiliki ni pamoja na DraftKings na Esports organisation Cloud9. Pia timu ya kikapu ya Los Angeles Sparks.
NYUMBA
Jamaa ameripotiwa kuwa na nyumba sehemu nyingi ambazo nyingine zimekuwa ni hoteli, ana nyumba kuanzia England ambako ana biashara zake lakini mbali ya mjengo huo, amejenga nyumba nyingine huko Marekani ambako muda mwingi yeye na famili yake ndio wanaishi na nyumba zote anazoishi zinakadiriwa kuwa na thamani ya dola 50 milioni.
MSAADA KWA JAMII
Amekuwa akisaidia jamii kupitia harambee na taasisi mbalimbali A family health condition led the Boehlys to learn of Focused ultrasound Foundation, The Dave Thomas Foundation, Finding a Cure for Epilepsy and Seizures (FACES), The Brunswick School na the Prostate Cancer Foundation.
MAISHA BINAFSI NA BATA
Yupo kwenye ndoa na mrembo Katie Boehly ambaye amefanikiwa kupata naye watoto watatu, tajiri haonekani sana kwenye fukwe za starehe na muda mwingi amekuwa bize na mambo ya kibishara.
USAFIRI
Ana usafiri wa magari makali yenye thamani kubwa na akiwa anafanya safari ya mbali huwa anaenda na ndege yake binafasi na jumla ya vyombo vya usafiri ambavyo anamiliki vinakadiriwa kufikia dola 20 milioni